باب فضل الجوع وخشونة العيش والاقتصار عَلَى القليل من المأكول والمشروب والملبوس وغيرها من حظوظ النفس وترك الشهوات
قَالَ الله تَعَالَى: ﴿وَمَا مِنْ دَابَّةٍ في الأرْضِ إِلاَّ عَلَى اللهِ رِزْقُهَا﴾ [ هود: 6 ]
وقال تَعَالَى: ﴿لِلْفُقَرَاءِ الَّذِينَ أُحْصِرُوا في سَبِيلِ اللهِ لاَ يَسْتَطِيعُونَ ضَرْباً فِي الأَرْضِ يَحْسَبُهُمُ الْجَاهِلُ أَغْنِيَاءَ مِنَ التَّعَفُّفِ تَعْرِفُهُمْ بِسِيمَاهُمْ لاَ يَسْأَلُونَ النَّاسَ إلْحَافاً﴾ [ البقرة: 273 ]،
وقال تَعَالَى: ﴿وَالَّذِينَ إِذَا أَنْفَقُوا لَمْ يُسْرِفُوا وَلَمْ يَقْتُرُوا وَكَانَ بَيْنَ ذَلِكَ قَوَاماً﴾ [ الفرقان: 67 ]
وقال تَعَالَى: ﴿وَمَا خَلَقْتُ الجِنَّ وَالإِنْسَ إِلاَّ لِيَعْبُدُونِ مَا أُرِيدُ مِنْهُمْ مِنْ رِزْقٍ وَمَا أُرِيدُ أَنْ يُطْعِمُونِ﴾ [ الذاريات: 56-57 ]
:وَأَمَّا الأحاديث، فتقدم معظمها في البابينِ السابقينِ، ومما لَمْ يتقدم
شرح الحديث على آيات الباب مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
57. MLANGO WA UKINAIFU, KUJIZUWIA KUOMBA, KUFANYA IKTISADI KATIKA MAISHA NA KATIKA KUTOA NA IZARA YA KUOMBA BILA DHARURA
Mwenyezi Mungu Amesema: [Na hakuna mnyama yoyote katika ardhi ila riziki yake iko kwa Allâh.” [11:6].
Mwenyezi Mungu Amesema: [ (Wapewe hizo sadaka) mafukara waliozuiwa katika Njia ya Allâh, wasioweza kwenda huko na huko katika ardhi (kufanya kazi ya kutafuta riziki); asiyewajua hali zao anadhania kuwa ni matajiri kwa sababu ya kujizuia kwao (na kuomba). Utawafahamu (kuwa wahitaji) kwa alama zao (zinazoonyesha ufukara, lakini) hawaombi watu wakafanya ung’ang’anizi.] [2:273].
Mwenyezi Mungu Amesema: [Na wale ambao wanapotumia hawatumii kwa fujo wala hawafanyi ubakhili, bali wanakuwa katikati baina ya hayo.” [25:67].
Mwenyezi Mungu Amesema: [ “Nami Sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi. Na Sitaki kwao riziki, wala Sitaki wanilishe.” [51:56, 57].