باب الإيثار والمواساة
وعن أَبي هريرة – رضي الله عنه -، قَالَ: قَالَ رسول الله – صلى الله عليه وسلم -: { طَعَامُ الاثْنَيْنِ كَافِي الثَّلاَثَةِ، وَطَعَامُ الثَّلاَثَةِ كَافِي الأربَعَةِ} متفقٌ عَلَيْهِ
وفي رواية لمسلمٍ عن جابر – رضي الله عنه -، عن النبي – صلى الله عليه وسلم -، قَالَ: { طَعَامُ الوَاحِدِ يَكْفِي الاثْنَيْنِ، وَطَعَامُ الاثْنَيْنِ يَكْفِي الأَرْبَعَةَ، وَطَعَامُ الأَرْبَعَة يَكْفِي الثَّمَانِية}
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa Abû Huraira (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Mtume ﷺ amesema: “Chakula cha watu wawili huwatosheleza watatu, na chakula cha watatu huwatosheleza wanne.” [ Wameafikiana Bukhari na Muslim.]
Riwaya nyingine ya Muslim, imepokewa kutoka kwa Jâbir (Radhi za Allah ziwe juu yake) kutoka kwa Mtume ﷺ amesema: “Chakula cha mtu mmoja huwatosheleza wawili, chakula cha wawili huwatosheleza wanne na chakula cha wanne huwatosheleza wanane.”