0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

563. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Kumtanguliza mwenzio na Kufarijian.

باب الإيثار والمواساة


وعن أَبي هريرة – رضي الله عنه -، قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النبيِّ – صلى الله عليه وسلم -، فَقَالَ: إنِّي مَجْهُودٌ، فَأرسَلَ إِلَى بَعْضِ نِسَائِهِ، فَقالت: وَالَّذي بَعَثَكَ بِالحَقِّ مَا عِنْدِي إِلاَّ مَاءٌ، ثُمَّ أرْسَلَ إِلَى أُخْرَى، فَقَالَتْ مِثلَ ذَلِكَ، حَتَّى قُلْنَ كُلُّهُنَّ مِثلَ ذَلِكَ: لا وَالَّذِي بَعَثَكَ بالحَقِّ مَا عِنْدِي إِلاَّ مَاءٌ. فَقَالَ النبي – صلى الله عليه وسلم -: { مَنْ يُضيفُ هَذَا اللَّيْلَةَ؟} فَقَالَ رَجُلٌ مِنَ الأنْصَارِ: أنَا يَا رسولَ الله، فَانْطَلَقَ بِهِ إِلَى رَحْلِهِ، فَقَالَ لامْرَأَتِهِ: أكرِمِي ضَيْفَ رسول الله – صلى الله عليه وسلم

وفي روايةٍ قَالَ لامْرَأَتِهِ: هَلْ عِنْدَكِ شَيْءٌ؟ فقَالَتْ: لاَ، إِلاَّ قُوتَ صِبيَانِي. قَالَ: فَعَلِّليهم بِشَيْءٍ وَإذَا أرَادُوا العَشَاءَ فَنَوِّمِيهمْ، وَإِذَا دَخَلَ ضَيْفُنَا فَأطْفِئي السِّرَاجَ، وَأريهِ أنَّا نَأكُلُ. فَقَعَدُوا وَأكَلَ الضَّيْفُ وَبَاتَا طَاوِيَيْنِ، فَلَمَّا أصْبَحَ غَدَا عَلَى النَّبيِّ – صلى الله عليه وسلم -، فَقَالَ: { لَقَدْ عَجبَ الله مِنْ صَنِيعِكُمَا بِضَيْفِكُمَا اللَّيْلَةَ}    متفقٌ عَلَيْهِ


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa Abû Huraira (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Alikuja mtu kwa Mtume , akamwambia: “Kwa hakika nina shida (mashaka na njaa kali).” Mtume akatumana kwa mkewe, akamjibu: “Naapa kwa Aliekutumiliza kwa haki, nilichonacho ni maji tu.” Kisha akatumana kwa mkewe mwingine, akajibu kama yule wa mwanzo, hata wote wakajibu vivyo hivyo: “Naapa kwa Aliekutumiliza kwa haki, nilichonacho ni maji tu.” Mtume ﷺ akauliza (Maswahaba): “Ni nani atakayemkaribisha huyu usiku huu?” Mtu mmoja katika Ansari akasema: “Mimi Yâ Rasûlallâh.” Akaenda naye nyumbani mwake. Akamwambia mkewe: “Mkirimu mgeni wa Mtume

 Riwaya nyingine imesema: “Akamwuliza mkewe: “Una kitu?” Akamjibu: “Sina, ispokuwa chakula cha wanangu.” Akamwambia: “Wapumbaze kwa kitu kingine, na watakapotaka chakula cha jioni walaze. Mgeni wetu atapoingia utazima taa na umuonyeshe kuwa sisi tunakula.” Wakaketi, mgeni akala na wao wakalala na njaa.” Kulipopambauka, alikwenda kwa Mtume , (Mtume) akamwambia: “Hakika Allâh Amekifurahikia kitendo chenu mlimchomfanyia mgeni wenu usiku huu!”   [ Wameafikiana Bukhari na Muslim.]

Begin typing your search above and press return to search.