باب الرجاء
قَالَ الله تَعَالَى: ﴿قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَى أَنْفُسِهِمْ لا تَقْنَطُوا مِنْ رَحْمَةِ اللهِ إِنَّ اللهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعاً إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴾ [ الزمر: 53 ]
وَقالَ تَعَالَى: ﴿ وَهَلْ نُجَازِي إِلاَّ الْكَفُور﴾ [ سـبأ: 17 ]
وَقالَ تَعَالَى: ﴿إِنَّا قَدْ أُوحِيَ إِلَيْنَا أَنَّ الْعَذَابَ عَلَى مَنْ كَذَّبَ وَتَوَلَّى﴾ [ طـه: 48 ]
وَقالَ تَعَالَى: ﴿وَرَحْمَتِي وَسِعَتْ كُلَّ شَيْءٍ﴾ [ الأعراف: 156 ]
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
51 MLANGO: KUTARAJI (REHMA ZA MWENYEZI MUNGU)
Mwenyezi Mungu Amesema:
[Sema: Enyi waja Wangu waliojidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Allâh. Hakika Allâh Husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.] [39: 53]
Mwenyezi Mungu Amesema:
[Nasi kwani Hatumwadhibu isipokuwa anayekufuru.] [34: 17].
Mwenyezi Mungu Amesema:
[ Nabii Mûsâ na Haruni wakasema:) Hakika tumefunuliwa sisi kwamba hapana shaka adhabu itamsibu anayekadhibisha na akapuuza.”] [20: 48].
Mwenyezi Mungu Amesema:
[ Na rehema Yangu imeenea kila kitu.] [7: 156].