باب فضل الحب في الله والحث عَلَيهِ وإعلام الرجل من يحبه، أنه يحبه، وماذا يقول لَهُ إِذَا أعلمه
قَالَ الله تَعَالَى: ﴿مُحَمَّدٌ رَسُولُ اللهِ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ( [الفتح: 29] إِلَى آخر السورة
وَقالَ تَعَالَى: ﴿وَالَّذِينَ تَبَوَّأُوا الدَّارَ وَالإِيمَانَ مِنْ قَبْلِهِمْ يُحِبُّونَ مَنْ هَاجَرَ إِلَيْهِمْ﴾ [الحشر: 9]
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
46 MLANGO WA FADHILA YA KUPENDA KWA AJILI YA ALLÂH NA MAHIMIZO YAKE; MTU KUMJULISHA ANAYEMPENDA KUWA YUWAMPENDA NA ANAYOTAKIWA KUMWAMBIA ATAKAPOJULISHWA HIVYO
Mwenyezi Mungu Amesema: [Muhammad ni Mtume wa Allâh. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao.] Mpaka mwisho wa Sura. [48: 29].
Mwenyezi Mungu Amesema: [Na (pia wapewe) wale waliofanya maskani yao (yaani Madina) na wakautaka Uislamu kabla ya (kuja) hao (Muhajirina huko Madina) na wakawapenda hao waliohamia kwao.]. [59: 9].