باب الرجاء
وعن أَبي هريرة أَوْ أَبي سعيد الخدري – رضي الله عنهما – – شك الراوي – ولا يَضُرُّ الشَّكُّ في عَين الصَّحَابيّ؛ لأنَّهُمْ كُلُّهُمْ عُدُولٌ – قَالَ: لَمَّا كَانَ غَزوَةُ تَبُوكَ، أصَابَ النَّاسَ مَجَاعَةٌ، فقالوا: يَا رَسُول الله، لَوْ أذِنْتَ لَنَا فَنَحرْنَا نَواضِحَنَا فَأكَلْنَا وَادَّهَنَّا ؟ فَقَالَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم –: {افْعَلُوا} فَجاء عُمَرُ – رضي الله عنه -، فَقَالَ: يَا رَسُول الله، إنْ فَعَلْتَ قَلَّ الظَّهْرُ، وَلَكِن ادعُهُمْ بفَضلِ أزْوَادِهِمْ، ثُمَّ ادعُ الله لَهُمْ عَلَيْهَا بِالبَرَكَةِ، لَعَلَّ الله أنْ يَجْعَلَ في ذلِكَ البَرَكَةَ. فَقَالَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -: {نَعَمْ} فَدَعَا بِنَطْع فَبَسَطَهُ، ثُمَّ دَعَا بِفضلِ أزْوَادِهِمْ، فَجَعَلَ الرَّجُلُ يَجيءُ بكَفّ ذُرَة وَيَجيءُ بِكَفّ تمر وَيجيءُ الآخرُ بِكِسرَة حَتَّى اجْتَمَعَ عَلَى النّطعِ مِنْ ذلِكَ شَيء يَسيرٌ، فَدَعَا رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم – بِالبَرَكَةِ، ثُمَّ قَالَ: {خُذُوا في أوعِيَتِكُمْ} فَأَخَذُوا في أوْعِيَتهم حَتَّى مَا تَرَكُوا في العَسْكَرِ وِعَاء إلاَّ مَلأوهُ وَأَكَلُوا حَتَّى شَبعُوا وَفَضَلَ فَضْلَةٌ فَقَالَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -: {أشْهَدُ أنْ لا إلهَ إلاَّ اللهُ وَأنّي رَسُولُ الله، لا يَلْقَى الله بِهِما عَبْدٌ غَيْرَ شَاكٍّ فَيُحْجَبَ عَنِ الجَنَّةِ} رواه مسلم
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa Abû Huraira au Abû Saîd al-Khudry (Radhi za Allah ziwe juu yako) – mpokezi amefanya shaka wala haidhuru kutia shaka kuhusu ni Swahaba yupi hasa ndiye alieipokea Hadîth hii kwa sababu wote ni waadilifu – amesimulia: “Ilipokuwa siku ya Vita vya Tabûk, watu walisibiwa na njaa. Wakamwambia Mtume ﷺ: “Yâ Rasûlallâh, (Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu) waonaje lau ukaturuhusu tuwachinje ngamia wetu, tule na tujipake mafuta yao?” Mtume ﷺ akawaambia: “Fanyeni.” ‘Umar (Radhi za Allah ziwe juu yake) akamwendea Mtume ﷺ , akamwambia: “Yâ Rasûlallâh, (Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu) ukiruhusu hivyo, wanyama watapungua. Lakini waite walete akiba ya chakula waliobakia nayo, halafu uwaombee Allâh Ateremshe baraka, huwenda Allâh Akajaalia baraka katika jambo hilo.” Mtume ﷺ akasema: “Sawa.” Akaitisha busati (la ngozi), akalikunjua, halafu akaitisha akiba ya chakula waliyonayo (Maswahaba). Basi ikawa mtu akija na konde la mahindi, mwengine akija na konde la tende na mwengine akileta kipande cha mkate, mpaka kikakusanyika kitu kichache katika busati lile. Mtume ﷺ akaombea baraka, kisha akawaambia: “Chukueni katika vyombo vyenu.” Maswahaba wakachukua wala hawakubakisha chombo katika jeshi ila walikijaza (chakula). Wakala mpaka wakashiba, na chakula kikabakia. Mtume ﷺ akasema: [Nashuhudia kuwa hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allâh na kwamba mimi ni Mtume wa Allâh. Mja yeyote atakayekutana na Allâh kwa maneno hayo mawili ilihali hana chembe ya shaka (moyoni mwake), hatazuiwa kuingia Peponi.] [ Imepokewa na Muslim.]