0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

33 DUA YA QUNUT YA WITR

KINGA YA MUISLAMU

اللّهُـمَّ اهْـدِنـي فـيمَنْ هَـدَيْـت، وَعـافِنـي فـيمَنْ عافَـيْت، وَتَوَلَّـني فـيمَنْ تَوَلَّـيْت ، وَبارِكْ لـي فـيما أَعْطَـيْت، وَقِـني شَرَّ ما قَضَـيْت، فَإِنَّـكَ تَقْـضي وَلا يُقْـضى عَلَـيْك إِنَّـهُ لا يَـذِلُّ مَنْ والَـيْت، [ وَلا يَعِـزُّ مَن عـادَيْت ]، تَبـارَكْـتَ رَبَّـنا وَتَعـالَـيْت

أخرجه أصحاب السنن الأربعة وأحمد والدرامي والحاكم والبيهقي

[Ewe Mwenyezi Mungu  niongoze pamoja na uliowaongoza, na unipe afya njema pamoja na uliowapa afaya njema, na nifanye kuwa ni mpenzi wako pamoja na uliowafanya  wapenzi na nibariki katika ulichonipa na nikinge na shari ya ulilolihukumu kwani Wewe unahukumu wala huhukumiwi.  Hakika hadhaliliki uliemfanya mpenzi (wala hatukuki uliemfanya adui ) Umetakasika Ewe Mola wetu na Umetukuka.]       [Imepokewa Kwenye vitabu vya Hadithi vinne na Ahmad na Al-Ddaarimiy na Hakim na Al-Bayhaqiy]

[ اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعـوذُ بِرِضـاكَ مِنْ  سَخَطِـك، وَبِمُعـافاتِـكَ مِنْ عُقوبَـتِك، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْـك، لا أُحْصـي ثَنـاءً عَلَـيْك، أَنْـتَ كَمـا أَثْنَـيْتَ عَلـى نَفْسـِك ]

أخرجه أصحاب السنن الأربعة وأحمد

[Ewe Mwenyezi Mungu  hakika mimi najilinda kwa radhi zako kutokana na hasira zako na kwa msamaha wako kutokana na adhabu yako, na najilinda  kwako kutokana na Wewe, mimi siwezi kuzidhibiti sifa zako, Wewe ni kama ulivyojisifu Mwenyewe.]       [Imepokewa na Abuu Daud na Al-Ttirmidhiy na Al-Nnasaai na Ibnu Maajah na Ahmad.]

اللّهُـمَّ إِيّـاكَ نعْـبُدْ، وَلَـكَ نُصَلّـي وَنَسْـجُد، وَإِلَـيْكَ نَسْـعى وَنَحْـفِد، نَـرْجو رَحْمَـتَك، وَنَخْشـى عَـذابَك، إِنَّ عَـذابَكَ بالكـافرين ملْحَـق. اللّهُـمَّ إِنّا نَسْتَعـينُكَ وَنَسْتَـغْفِرُك، وَنُثْـنـي عَلَـيْك الخَـيْرَ، وَلا نَكْـفُرُك، وَنُـؤْمِنُ بِك، وَنَخْـضَعُ لَكَ وَنَخْـلَعُ مَنْ يَكْـفرُك

 أخرجه البيهقي في السنن الكبرى وصحح إسناده

[Ewe Mwenyezi Mungu , Wewe tu ndie tunaekuabudu, na kwako tunasali na tunasujudu, na kwako tunakimbilia na tunakutumikia, tunataraji rehema yako na tunaogopa adhabu yako, kwani adhabu yako hakuna shaka kuwa makafiri itawifikia.  Ewe Mwenyezi Mungu  hakika sisi tunakutaka msaada na tunakutaka msamaha na tunakusifu kwa kheri na wala hatukukufurishi na tunakuamini Wewe, na tunakunyenyekea na tunamuepuka anaekukufuru.]      [Imepokewa na Al-Bayhaqiy katika Al-Ssunanul-Kubra na kasahihisha isnadi yake.]


SIKILIZA DUA YA QUNUT YA WITR


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.