باب بر الوالدين وصلة الأرحام
وعن أَبي عبد الرحمان عبد الله بن مسعود – رضي الله عنه -، قَالَ: سألت النبي – صلى الله عليه وسلم -: أيُّ العَمَلِ أحَبُّ إِلَى اللهِ تَعَالَى؟ قَالَ: {الصَّلاةُ عَلَى وَقْتِهَا}، قُلْتُ: ثُمَّ أي؟ قَالَ: {بِرُّ الوَالِدَيْنِ}، قُلْتُ: ثُمَّ أيٌّ؟ قَالَ: {الجِهَادُ في سبيلِ الله} مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa Abû ‘Abdirrahmân, ‘Abdullâh bin Mas‘ûd Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: “Nilimwuliza Mtume ﷺ: “Ni amali gani inayopendeza zaidi kwa Allâh? Akajibu: [Ni kuswali kwa wakati wake.] Nikamwuliza tena: Kisha ni amali gani? Akajibu: [Ni kuwafanyia hisani wazazi. ] Nikamwuliza tena: Kisha ni amali gani? Akajibu: [Ni kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.] [Wameafikiana Bukhari na Muslim]