BUSTANI YA WATU WEMA
وعن أَبي حفص عمر بن أَبي سلمة عبد الله بن عبد الأسدِ ربيبِ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -، قَالَ: كُنْتُ غلاَماً في حجر رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم – وَكَانَتْ يَدي تَطِيشُ في الصَّحْفَةِ، فَقَالَ لي رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -: {يَا غُلامُ، سَمِّ الله تَعَالَى، وَكُلْ بيَمِينكَ، وَكُلْ مِمَّا يَلِيكَ} فَمَا زَالَتْ تِلْكَ طِعْمَتي بَعْدُ. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
{وَتَطِيشُ}: تدور في نواحِي الصحفة
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa Abû Hafs ‘Umar bin Abî Salamah, ‘Abdullâh bin ‘Abdil-asad Radhi za Allah ziwe juu yake ambaye ni mwanakambo wa Mtume ﷺ , amesimulima: “Nilikuwa kijana mdogo chini ya malezi ya Mtume ﷺ , na mkono wangu ulikuwa ukizunguka-zunguka katika sinia (ya chakula). Mtume ﷺ akaniambia: “Ee kijana, taja Jina la Allâh, ule kwa mkono wako wa kulia na ule kilicho mbele yako.” Basi huo ukawa ndio mtindo wangu wa kula baadaye” [Wameafikiana Bukhari na Muslim].