BUSTANI YA WATU WEMA
وعن عبد الله بن زَمْعَةَ – رضي الله عنه -: أنَّهُ سَمِعَ النَّبيّ – صلى الله عليه وسلم – يَخْطُبُ، وَذَكَرَ النَّاقَةَ وَالَّذِي عَقَرَهَا، فَقَالَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -: {﴿إِذ انْبَعَثَ أشْقَاهَا﴾ انْبَعَثَ لَهَا رَجُلٌ عَزيزٌ، عَارِمٌ مَنيعٌ في رَهْطِهِ}، ثُمَّ ذَكَرَ النِّسَاءَ، فَوعَظَ فِيهنَّ، فَقَالَ: {يَعْمِدُ أحَدُكُمْ فَيَجْلِدُ امْرَأتَهُ جَلْدَ العَبْدِ فَلَعَلَّهُ يُضَاجِعُهَا مِنْ آخِرِ يَومِهِ} ثُمَّ وَعَظَهُمْ في ضَحِكِهمْ مِنَ الضَّرْطَةِ، وَقالَ: {لِمَ يَضْحَكُ أَحَدُكُمْ مِمَّا يَفْعَلُ؟! } مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa Abdullâh bin Zam‘ah Radhi za Allah ziwe juu yake amesimulia kuwa alimsikia Mtume ﷺ akikhutubu, akamtaja ngamia (wa Nabii Swaleh) na aliemchinja. Mtume ﷺ akasema: [Aliposimama muovu wao mkubwa (ili kumchinja ngamia huyo wa miujiza). Alisimama mtu mwenye iza aliye muovu fisadi mwenye kinga ya watu wake (akamchinja)] Kisha akagusia wanawake, akatoa waadhi kuhusu wao, akasema: [Mmoja wenu anampiga mkewe kama anavyomchapa mtumwa na pengine akalala naye mwisho wa siku hiyo (aliyompiga)] Halafu akawapa mawaidha kuhusiana na kucheka kwao kwa sababu ya kushuta (kujamba), akasema: [Mbona mmoja wenu anacheka kwa jambo analolifanya?] [Wameafikiana Bukhari na Muslim]