BUSTANI YA WATU WEMA
وعن أَبي قَتَادَةَ الْحارثِ بنِ ربعي رضي اللَّه عنه عن رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم أَنَّهُ قَام فِيهمْ، فذَكَرَ لَهُمْ أَنَّ الْجِهادَ فِي سبِيلِ اللَّه ، وَالإِيمانَ بِاللَّه أَفْضلُ الأَعْمالِ، فَقَامَ رَجلٌ فقال: يا رسول اللَّه أَرَأَيْت إِنْ قُتِلْتُ فِي سَبِيلِ اللَّه ، تُكَفِّرُ عنِي خَطَايَاىَ؟ فقال لَهُ رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : « نعَمْ إِنْ قُتِلْتَ فِي سَبِيلِ اللَّه وأَنْتَ صَابر مُحْتَسِبٌ ، مُقْبِلٌ غيْرَ مُدْبرٍ » ثُمَّ قال رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : « كيْف قُلْتَ ؟ » قال : أَرَأَيْتَ إِنْ قُتِلْتُ فِي سَبِيل اللَّه ، أَتُكَفرُ عني خَطَاياي ؟ فقال رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : «نَعمْ وأَنْت صابِرٌ مُحْتَسِبٌ ، مُقبِلٌ غَيْرَ مُدْبِرٍ ، إِلاَّ الدَّيْن فَإِنَّ جِبْرِيلَ قال لِي ذلِكَ » رواه مسلم
Kutoka kwa Abuu Qataadah bin Al-Haarith bin Rab’iyy Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume ﷺ alisimama mbele yao, akawatajia kuwa jihaad katika njia ya Mwenyezi Mungu na kumuamini Mwenyezi Mungu ndio ‘amali bora. Alisimama mtu mmoja akasema: Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu! Waonaje nikiuliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu nitasamehewa madhambi yangu? Mtume ﷺ akamwambia: [Ndio, ukiuliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu nawe ukawa katika hali ya kusubiri na huku unatarajia malipo ukiwa unasonga mbele katika vita wala sio kurudi nyuma (na kukimbia).] Kisha Mtume ﷺ akamuliza: [Umesema nini?] Akasema: Ee Rasuli wa Mwenyezi Mungu! Waonaje nikiuliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu nitasamehewa makossa yangu? Mtume ﷺ akasema: [Ndio, ukiuliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu nawe ukawa katika hali ya kusubiri na huku watarajia malipo (kutoka kwa Allaah), ukiwa unasonga mbele katika vita wala sio kurudi nyuma ila (ukiwa na) deni Hakika Jibril ameniambia hilo.] [Imepokewa na Muslim]
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله