0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

218. Riyadhu Swalihina Mlango wa Uharamu wa kudhulumu na Amri ya kurudisha Vilivyodhulumiwa Hadithi 16

BUSTANI YA WATU WEMA


وعن أَبي هريرة رضي اللَّه عنه ، أَن رسولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال : «أَتَدْرُون من الْمُفْلِسُ ؟» قالُوا : الْمُفْلسُ فِينَا مَنْ لا دِرْهَمَ لَهُ وَلا مَتَاعَ . فقال : « إِنَّ الْمُفْلِسَ مِنْ أُمَّتِي مَنْ يَأْتِي يَوْمَ الْقيامةِ بِصَلاةٍ وَصِيَامٍ وزَكَاةٍ ، ويأْتِي وقَدْ شَتَمَ هذا ، وقذَف هذَا وَأَكَلَ مالَ هَذَا، وسفَكَ دَم هذَا ، وَضَرَبَ هذا ، فيُعْطَى هذَا مِنْ حسَنَاتِهِ ، وهَذا مِن حسَنَاتِهِ ، فَإِنْ فَنِيَتْ حسناته قَبْلَ أَنْ يقْضِيَ مَا عَلَيْهِ ، أُخِذَ مِنْ خَطَايَاهُمْ فَطُرحَتْ علَيْه ، ثُمَّ طُرِح في النَّارِ»    رواه مسلم


Kutoka kwa Abuu Hurayrah Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema: [Je, mnamjua Muflis?]  (Maswahaba) Wakasema: Muflis kwetu sisi ni yule asiyekuwa na dirham wala mali. Akasema: [Hakika Muflis katika Umma wangu ni yule atakayekuja Siku ya Qiyama akiwa ana Swala, Saum, na Zakaa. Na anakuja akiwa amemtusi huyu, na amemsingizia uzinifu huyu, amekula mali ya huyu, amemwaga damu ya huyu na kumpiga huyu. Kila mmoja (katkika waliodhulumia) atapewa sehemu ya mema yake, na yule atapewa sehemu ya mema yake. Mema yake yatakapomalizika kabla ya kulipa anayodaiwa, zitachukuliwa sehemu ya dhambi zao (kulingana na alivyo dhulumu) na apewe yeye, kisha atupwe motoni.]    [Imepokewa na Muslim]


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله



Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.