0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

213. Riyadhu Swalihina Mlango wa Uharamu wa kudhulumu na Amri ya kurudisha Vilivyodhulumiwa Hadithi 11


BUSTANI YA WATU WEMA


1463655589


وعن أَبي بَكْرَةَ نُفَيْعِ بنِ الحارثِ رضيَ اللَّه عنهُ عن النبي صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال: « إِنَّ الزَّمَانَ قَدِ اسْتَدَارَ كَهَيْئَتِهِ يَوْمَ خَلَقَ اللَّه السَّمواتِ والأَرْضَ : السَّنةُ اثْنَا عَشَر شَهْراً ، مِنْهَا أَرْبَعَةٌ حُرُم: ثَلاثٌ مُتَوَالِيَاتٌ : ذُو الْقعْدة وَذو الْحِجَّةِ ، والْمُحرَّمُ ، وَرجُب الذي بَيْنَ جُمادَي وَشَعْبَانَ ، أَيُّ شَهْرٍ هَذَا ؟ » قلْنَا : اللَّه ورسُولُهُ أَعْلَم ، فَسكَتَ حَتَّى ظنَنَّا أَنَّهُ سَيُسمِّيهِ بِغَيْرِ اسْمِهِ ، قال : أَليْس ذَا الْحِجَّةِ ؟ قُلْنَا : بلَى: قال : « فأَيُّ بلَدٍ هَذَا ؟ » قُلْنَا: اللَّه وَرسُولُهُ أَعلمُ ، فَسَكَتَ حتَّى ظَنَنَّا أَنَّهُ سيُسمِّيهِ بغَيْر اسْمِهِ . قال : « أَلَيْسَ الْبلْدةَ الحرمَ ؟ » قُلْنا : بلَى . قال : « فَأَيُّ يَومٍ هذَا ؟ » قُلْنَا : اللَّه ورسُولُهُ أَعْلمُ ، فَسكَتَ حَتَّى ظَنَنَّا أَنَّه سيُسمِّيهِ بِغيْر اسمِهِ . قال : « أَلَيْسَ يَوْمَ النَّحْر ؟ » قُلْنَا : بَلَى . قال : « فإِنَّ دِماءَكُمْ وَأَمْوَالَكُمْ وأَعْراضَكُمْ عَلَيْكُمْ حرَامٌ ، كَحُرْمَةِ يَوْمِكُمْ هَذَا في بَلَدِكُمْ هَذا في شَهْرِكم هَذَا ، وَسَتَلْقَوْن ربَّكُم فَيَسْأْلُكُمْ عَنْ أَعْمَالِكُمْ ، أَلا فَلا تَرْجِعُوا بَعْدِي كُفَّاراً يضْرِبُ بَعْضُكُمْ رِقَابَ بَعْضٍ ، أَلاَ لِيُبلِّغِ الشَّاهِدُ الْغَائِبَ ، فلَعلَّ بعْض من يبْلغُه أَنْ يَكُونَ أَوْعَى لَه مِن بَعْضِ مَنْ سَمِعه » ثُمَّ قال : « أَلا هَلْ بَلَّغْتُ ، أَلا هَلْ بلَّغْتُ ؟ » قُلْنا : نَعَمْ ، قال : « اللَّهُمْ اشْهدْ »    متفقٌ عليه


Kutoka kwa  Abu Bakr Nufay’ bin Haarith kuwa Mtume amesema: [Hakika zama (mwaka) zimegeuka kama siku alivyo umba Mwenyezi Mungu mbingu na ardhi: Mwaka una miezi kumi na mbili, miongoni mwayo ni miezi minne iliyo mitukufu. Miezi mitatu ni ya kufuatana: Dhul Qa’dah, Dhul Hijjah na Muharram na Rajab, mwezi ambao upo baina ya Jumaadah na Sha’baani.] Kisha akauliza: [Je, huu ni mwezi gani?] Wakasema (Maswahaba): Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanajua zaidi. Mtume ﷺ akanyamaza mpaka tukadhania atauita kwa jina lingine. Akasema: [Je, huu si mwezi wa Dhul Hijjah?] Tukasema: Ndio. Akauliza: [Je, huu ni mji gani?] Tukasema: Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanajua zaidi. Mtume ﷺ akanyamaza mpaka tukadhania atauita kwa jina lingine lisilikuwa jina lake. Akasema: [Je, huu si mji wa (Makkah)?] Tukasema: Ndio. Akasema: [Je, hii ni siku gani?] Tukasema: Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanajua zaidi. Mtume ﷺ akanyamaza mpaka tukadhania kuwa ataiita kwa jina lingine. Akasema: [Je, hii si ni siku ya kuchinja?] Tukasema: Ndio. Akasema: [Hakika damu zenu, mali zenu, na heshima zenu ni haramu kwenu kama uharamu (wa kufanya dhambi) siku yenu hii, katika mji wenu huu, katika mwezi wenu huu. Na bila shaka mtakutana na Mola wenu na kuwauliza juu ya Amali zenu. Fahamuni! Msirudi baada yangu katika ukafiri mkiuana ninyi kwa ninyi. Jueni! Aliyehudhuria amfikishie asiyekuwepo, huenda baadhi ya watakao fikishiwa wakawa wanafahamu nzuri zaidi kuliko waliosikia.] Kisha akauliza: [Je, nimefikisha?] Tukasema: Ndio. Akasema: [Ee Mwenyezi Mungu shuhudia]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim]


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله



Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.