0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

202. Riyadhu Swalihina Mlango wa Maamrisho ya kutekeleza Amana Hadithi 04


BUSTANI YA WATU WEMA


1463655589


وعن أَبِي خُبَيْبٍ بضم الخاءِ المعجمة  عبد اللَّهِ بنِ الزُّبَيْرِ ، رضي اللَّه عنهما قال : لَمَّا وَقَفَ الزبَيْرُ يَوْمَ الْجَمَلِ دَعانِي فَقُمْتُ إِلَى جَنْبِهِ ، فَقَالَ : يَا بُنَيَّ إِنَّهُ لا يُقْتَلُ الْيَوْمَ إِلاَّ ظَالِمٌ أَوْ مَظْلُومٌ ، وإِنِّي لاأُرَنِي إِلاَّ سَأُقْتَلُ الْيَومَ مَظْلُوماً، وَإِنَّ مِنْ أَكْبَرِ هَمِّي لَدَينْيِ أَفَتَرَى دَيْنَنَا يُبْقى مِنْ مالنا شَيْئاً ؟ ثُمَّ قَالَ : بعْ مَالَنَا واقْضِ دَيْنِي ، وَأَوْصَى بالثُّلُثِ ، وَثُلُثِهُ لبنيه ، يَعْنِي لبَنِي عَبْدِ اللَّه بن الزبير ثُلُثُ الثُّلُث . قَالَ : فَإِن فَضلِ مِنْ مالِنَا بعْدَ قَضَاءِ الدَّيْنِ شَيءٌ فثُلُثُهُ لِبَنِيك ، قَالَ هِشَامٌ : وكان وَلَدُ عَبْدِ اللَّهِ قَدْ ورأى بَعْضَ بَني الزبَيْرِ خُبيبٍ وَعَبَّادٍ ، وَلَهُ يَوْمَئذٍ تَسْعَةُ بَنينَ وتِسعُ بَنَاتٍ . قَالَ عَبْدُ اللَّه : فَجَعَل يُوصِينِي بديْنِهِ وَيَقُول : يَا بُنَيَّ إِنْ عَجزْتَ عنْ شَيءٍ مِنْهُ فَاسْتَعِنْ عَلَيْهِ بموْلايَ . قَالَ : فَوَاللَّهِ مَا دَريْتُ ما أرادَ حَتَّى قُلْتُ  يَا أَبَتِ مَنْ مَوْلاَكَ ؟ قَالَ : اللَّه . قال : فَواللَّهِ مَا وَقَعْتُ في كُرْبَةٍ مِنْ دَيْنِهِ إِلاَّ قُلْتُ: يَا مَوْلَى الزبَيْرِ اقض عَنْهُ دَيْنَهُ ، فَيَقْضِيَهُ . قَالَ : فَقُتِلَ الزُّبَيْرُ وَلَمْ يَدَعْ دِينَاراً وَلاَ دِرْهَماً إِلاَّ أَرَضِينَ ، مِنْهَا الْغَابَةُ وَإِحْدَى عَشَرَةَ داراً بالْمَدِينَةِ . وداريْن بالْبَصْرَةِ ، وَدَارَاً بالْكُوفَة وَدَاراً بِمِصْرَ . قال : وَإِنَّمَا كَانَ دَيْنُهُ الذي كَانَ عَلَيْهِ أَنَّ الرَّجُلَ يَأْتَيهِ بِالمالِ ، فَيَسْتَودِعُهُ إِيَّاهُ ، فَيَقُولُ الزُّبيْرُ: لا وَلَكنْ هُوَ سَلَفٌ إِنِّي أَخْشَى عَلَيْهِ الضَّيْعةَ . وَمَا ولِي إَمَارَةً قَطُّ وَلا جِبَايةً ولا خَراجاً ولا شَيْئاً إِلاَّ أَنْ يَكُونَ في غَزْوٍ مَعَ رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، أَوْ مَعَ أَبِي بَكْر وَعُمَرَ وَعُثْمَانَ رضي اللَّه عنهم ، قَالَ عَبْدُ اللَّه : فَحَسَبْتُ مَا كَانَ عَلَيْهِ مِنَ الدَّيْنِ فَوَجَدْتُهُ أَلْفَيْ أَلْفٍ وَمائَتَيْ أَلْفٍ، فَلَقِيَ حَكِيمُ بْنُ حِزَامٍ عَبدَ اللَّهِ بْن الزُّبَيْرِ فَقَالَ : يَا ابْنَ أَخِي كَمْ عَلَى أَخِي مِنَ الدَّيْنِ ؟ فَكَتَمْتُهُ وَقُلْتُ : مِائَةُ أَلْفٍ . فَقَالَ : حَكيمٌ : وَاللَّه مَا أَرى أَمْوَالَكُمْ تَسعُ هَذِهِ ، فَقَالَ عَبْدُ اللَّهِ : أَرَأَيْتُكَ إِنْ كَانَتْ أَلْفَي أَلْفٍ ؟ وَمِائَتَيْ أَلْفٍ ؟ قَالَ : مَا أَرَاكُمْ تُطِيقُونَ هَذَا ، فَإِنْ عَجَزْتُمْ عَنْ شَىْء مِنْهُ فَاسْتَعِينُوا بِي . قَالَ : وكَانَ الزُّبَيْرُ قدِ اشْتَرَى الْغَابَةَ بِسَبْعِينَ ومِائَة أَلْف، فَبَاعَهَا عَبْدُ اللَّهِ بِأْلف ألفٍ وسِتِّمِائَةِ أَلْفَ ، ثُمَّ قَامَ فَقالَ : مَنْ كَانَ لَهُ عَلَى الزُّبَيْرِ شَيْء فَلْيُوافِنَا بِالْغَابَةِ ، فأَتَاهُ عبْدُ اللَّهِ بْنُ جَعفر ، وكَانَ لَهُ عَلَى الزُّبَيْرِ أَرْبعُمِائةِ أَلْفٍ ، فَقَالَ لعَبْدِ اللَّه : إِنْ شِئْتُمْ تَرَكْتُهَا لَكُمْ ؟ قَالَ عَبْدُ اللَّه : لا ، قال فَإِنْ شِئْتُمْ جعَلْتُمْوهَا فِيمَا تُؤخِّرُونَ إِنْ أَخَّرْتُمْ ، فقال عَبْدُ اللَّه : لا ، قال : فَاقْطَعُوا لِي قِطْعَةً ، قال عبْدُ اللَّه : لَكَ مِنْ هاهُنا إِلَى هاهُنَا. فَبَاعَ عَبْدُ اللَّهِ مِنْهَا فَقَضَى عَنْهُ دَيْنَه ، وَوَفَّاهُ وَبَقِيَ منْهَا أَرْبَعةُ أَسْهُمٍ وَنِصْفٌ ، فَقَدم عَلَى مُعَاوِيَةَ وَعَنْدَهُ عَمْرُو بْنُ عُثْمَانَ ، وَالْمُنْذِرُ بْنُ الزُّبيْرِ ، وَابْن زَمْعَةَ . فقال لَهُ مُعَاوِيَةُ : كَمْ قَوَّمَتِ الْغَابَةُ ؟ قال : كُلُّ سَهْمٍ بِمائَةِ أَلْفٍ قال: كَمْ بَقِي مِنْهَا ؟ قال : أَرْبَعَةُ أَسْهُمٍ ونِصْفٌ ، فقال الْمُنْذرُ بْنُ الزَّبَيْرِ : قَدْ أَخَذْتُ مِنْهَا سَهْماً بِمائَةِ أَلْفٍ ، وقال عَمْرُو بنُ عُثْمان : قَدْ أَخَذْتُ مِنْهَا سَهْماً بِمِائَةِ أَلْفٍ . وقال ابْن زمْعَةَ : قَدُ أَخَذْتُ مِنها سَهْماً بِمِائَةِ أَلْفٍ ، فَقَالَ مُعَاوِيةُ : كَمْ بَقِيَ مِنْهَا؟ قال : سَهْمٌ ونصْفُ سَهْمٍ ، قَالَ : قَدْ أَخَذْتُهُ بِخَمسينَ ومائَةِ ألف . قَالَ : وبَاعَ عَبْدُ اللَّه بْنُ جَعْفَرٍ نصِيبَهُ مِنْ مُعَاوِيَةَ بسِتِّمِائَةِ أَلْفٍ. فَلَمَّا فَرغَ ابنُ الزُّبَيْرِ مِنْ قََضاءِ ديْنِهِ قَالَ بَنُو الزُّبْيرِ : اقْسِمْ بَيْنَنَا مِيراثَنَا . قَالَ : وَاللَّهِ لا أَقْسِمُ بيْنَكُمْ حَتَّى أَنَادِيَ بالموسم أَرْبَع سِنِين : أَلا مَنْ كان لَهُ عَلَى الزُّبَيَّرِ دَيْنٌ فَلْيَأْتِنَا فَلْنَقْضِهِ . فَجَعَلَ كُلُّ سَنَةٍ يُنَادِي في الْمَوسمِ ، فَلَمَّا مَضى أَرْبَعُ سِنينَ قَسم بَيْنَهُمْ ودَفَعَ الثُلث وكَان للزُّبَيْرِ أَرْبَعُ نِسْوةٍ ، فَأَصاب كُلَّ امْرَأَةٍ أَلْفُ أَلْفٍ ومِائَتَا أَلْفٍ ، فَجَمِيعُ مَالِهِ خَمْسُونَ أَلْف أَلْفٍ ومِائَتَا أَلْف.    رواه البخاري


Kutoka kwa Abuu Khubayd, ‘Abdullaah bin Az-Zubayr Radhi za Allah ziwe juu yao Amesema: Aliposimama Az-Zubayr katika vita vya Ngamia, aliniita nami nikasimama ubavuni mwake. Alinambia: Ewe mtoto wangu! Hautauliwa leo isipokuwa dhalimu au aliyedhulumiwa. Nami nina hakika ya kuwa nitauliwa nikiwa nimedhulumiwa. Na hakika hamu yangu kubwa ni deni langu. Je, unafikiria kutabakia chochote katika mali baada ya kulipa deni? Kisha akasema: Ewe mtoto wangu! Uza rasimali yangu na ulipe deni langu. Na nausia ya kwamba thuluthi ya thuluthi (1/9) iwe ni ya watoto wako (yaani ‘Abdullaah bin Az-Zubayr), kwa kile kitakachobakia. Baada ya hii ikiwa kutabakia chochote basi thuluthi itakuwa ni ya watoto wako. Amasema Hishaam: Na walikuwa baadhi ya watoto wa ‘Abdullaah ni rika moja na watoto wa Az-Zubayr, kama Khubayb na ‘Abbaad, na wakati huo alikuwa na vijana tisa na mabinti tisa. Akasema: Ewe mtoto wangu! Ukishindwa kulipa deni langu basi takamsaada kwa Bwana wangu. Akasema: Naapa kwa Mwenyezi Mungu! Sikufahamu alilokusudia mpaka nilipouuliza: Ewe baba yangu! Nani bwana wako? Akasema: ni Mwenyezi Mungu. Akasema tena (‘Abdullaah): Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu! Sijapatwa tena na shida ya deni lake isipokuwa nilikuwa nasema, Ee Bwana wa Az-Zubayr mwondoshee deni lake, Naye Allaah (Subhaanahu Wa Ta’aalaa) Alikuwa anamuondoshea. Az-Zubayr Radhi za Allah ziwe juu yake aliuliwa siku hiyo na hakuacha hata dinari moja wala dirhamu isipokuwa vipande viwili vya ardhi, moja katika hiyo ikiwa katika sehemu ya Ghaabah na nyumba kumi na moja Madina, na nyumba mbili Basrah, na nyumba moja Kufah, na nyumba moja Misri. Na kwa hakika deni lake lilitokana na watu waliokuwa wakimjia ili awahifadhie mali zao, lakini Az-Zubayr alikuwa anawaambia: Hapana! Siwezi jukumu hilo kwani huenda ikapotea lakini naweza kuichukua hiyo amana kama deni juu yangu. Yeye hakukubali nafasi ya uongozi wala wadhifa wa kukusanya kodi wala kitu chengine chochote isipokuwa ile ngawira aliyopatiwa katika vita alivyopigana wakati wa Mtume ﷺ, au Abu Bakr, au ‘Umar, au ‘Uthmaan Radhi za Allah ziwe juu yao. Akasema (‘Abdullaah): Nikahesabu deni lake na jumla ikafika million mbili na laki mbili. Nilikutana na Hakiym bin Hizaam, naye akasema: Ewe mtoto wa ndugu yangu! Ndugu yangu anadenia la kiasi gani? Nikaficha hilo kwa kusema: Laki moja. Akasema Hakiym: Kwa Allaah, sidhani ya kwamba mali yenu itafikia kiwango hicho. Nikasema: Unaonaje deni likiwa ni milioni mbili na laki mbili? Akasema: Sidhani ya kwamba mtaweza kuubeba mzigo huo, hivyo mkiwa na uzito wa aina yoyote njooni kwangu kwa msaada. Az-Zubayr alikuwa ameinunua ile ardhi ya Ghaabah kwa laki moja na elfu sabini, nami nikauza kwa milioni moja na laki sita. Kisha akasimama ‘Abdullaah na kunadi Az-Zubayr atukute katika ardhi ya Ghaabah. Akaja ‘Abdullaah bin Ja’far, ambaye alikuwa anamdai Az-Zubayr laki nne. Alimwambia ibn Zubayr: Mkipenda nitawaachia deni hilo? Nikasema: Hapana, Akasema: Ikiwa mnataka nitawapatia muda wa kunilipa. Akasema ibn Zubayr: Hapana. Akasema ibn Ja’far basi nikatie kipande cha ardhi. Akasema ‘Abdullaah: Kipande chako ni kuanzia hapa mpaka hapa. Kwa njia hii ‘Abdullaah alimlipia baba yake deni. Baada ya hapo ikabaki ardhi yenye kipimo cha siham nne na nusu. Akaja Mu’awiyyah pamoja naye ni ‘Amru bin ‘Uthmaan na Al-Mundhir bin Az-Zubayr na ibn Zam’ah. Akasema Mu’awiyyah: Hii Ghaabah ni bei gani? Akasema: Kila siham ni laki moja. Akasema: Imebakia kiasi gani? Akasema: Siham nne na nusu. Hapo akasema Mundhir bin Zubayr: Mimi nimechukua sihim moja kwa bei hiyo ya laki moja. Akasema ‘Amru bin ‘Uthmaan: Nami nachukua sihim moja kwa bei hiyo ya laki moja. Na akasema ibn Zam’ah: Nami nimechukua sihim moja kwa bei ya laki moja. Akasema Mu’awiyyah: Imebaki kiasi gani cha ardhi? Akasema (‘Abdullaah): Sihim moja na nusu. Akasema Mu’awiyyah: Nimeichukua kwa laki moja na nusu. Baadae ‘Abdullaah bin Ja’far alimuuzia Mu’awiyyah sehemu yake ya ardhi kwa laki sita. ‘Abdullaah bin Zubayr alipomaliza shughuli hii yote ya kulipa madeni ya baba yake, walimjia warithi wa Az-Zubayr  na kumwambia: Tupatie fungu letu la mirathi. Akasema: Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu! Sitagawa mirathi mpaka mwanzo ninadi katika msimu wa Hijjah kwa miaka minne mfululizo. Mtu yoyote anayemdai Az-Zubayr basi atujie tumrudishie haki yake. Akajaalia kuwa ananadi kila mwaka katika msimu wa Hijjah. Ilipomalizika miaka minne aligawanya pesa zilizobakia baina yao akalipa thuluthi. Az-Zubayr alikuwa na wake wanne, hivyo kila mmke alipata milioni moja na laki mbili, kwani jumla ya mali yake yote ilikuwa milioni khamsini na laki mbili.   [Imepokewa na Bukhari]


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله





Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.