0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

176. Riyadhu Swalihina Mlango wa Kujulisha kheri na kulingania katika Uongofu au Upotevu Hadithi 04

BUSTANI YA WATU WEMA


وعن أَنسٍ رضي اللَّه عنه أَنْ فَتًى مِنْ أَسْلَمَ قال : يا رسُولَ اللَّه إِنِّي أُرِيد الْغَزْوَ ولَيْس مَعِي مَا أَتجهَّزُ بِهِ ؟ قَالَ : « ائْتِ فُلاناً فإِنه قَدْ كانَ تَجَهَّزَ فَمَرِضَ »  فَأَتَاهُ فقال : إِنَّ رسولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يُقْرئُكَ السَّلامَ وَيَقُولُ : أَعْطِني الذي تجَهَّزْتَ بِهِ ، فقال : يا فُلانَةُ أَعْطِيهِ الذي تجَهَّزْتُ بِهِ ، ولا تحْبِسِي مِنْهُ شَيْئاً ، فَواللَّه لا تَحْبِسِينَ مِنْهُ شَيْئاً فَيُبَارَكَ لَكِ فِيهِ . رواه مسلم


Kutoka kwa Anas bin Maalik Radhi za Allah ziwe juu yake  ya kwamba kijana katika kabila la Aslam alikuja na kusema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ! Mimi ninataka kushiriki katika vita, lakini sina chochote cha kujitayarisha kwayo?”  Mtume ﷺ akamwambia : [Nenda kwa Fulani kwani yeye alikuwa amejitayarisha akawa mgonjwa.]  Huyu kijana akaenda kwa huyo mtu na kumwambia: “Kwa hakika Mtume  anakutolea salamu na anakwambia: Nipatie mimi vifaa ulivyovitayarisha ili kuvitumia katika vita.” Akasema yule Fulani: “Ewe mke wangu mpatie kila kitu nilichotayarisha wala usibakishe chochote. Naapa kwa jina la Allaah, hutabakisha kitu chochote kisha Mwenyezi Mungu akubarikie kwa kitu hicho .”    [Imepokewa na Muslim]


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله



Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.