0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

175. Riyadhu Swalihina Mlango wa Kujulisha kheri na kulingania katika Uongofu au Upotevu Hadithi 03

BUSTANI YA WATU WEMA


وعن أَبي العباسِ سهل بنِ سعدٍ السَّاعِدِيِّ  رضي اللَّه عنه أَن رسولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال يَوْمَ خَيْبَرَ : « لأعْطِيَنَّ الرَّايَةَ غَداً رَجُلاً يَفْتَحُ اللَّه عَلَى يَدَيْهِ ، يُحبُّ اللَّه ورسُولَهُ ، وَيُحبُّهُ اللَّه وَرَسُولُهُ » فَبَاتَ النَّاسُ يَدُوكونَ لَيْلَتَهُمْ أَيُّهُمْ يُعْطَاهَا . فَلَمَّا أصبحَ النَّاسُ غَدَوْا عَلَى رسولِ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : كُلُّهُمْ يَرجُو أَنْ يُعْطَاهَا ، فقال: « أَيْنَ عليُّ بنُ أَبي طالب ؟ » فَقيلَ : يا رسولَ اللَّه هُو يَشْتَكي عَيْنَيْه قال : « فَأَرْسِلُوا إِلَيْهِ » فَأُتِي بِهِ ، فَبَصقَ رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم في عيْنيْهِ ، وَدعا لَهُ ، فَبَرأَ حَتَّى كَأَنْ لَمْ يَكُنْ بِهِ وَجعٌ ، فأَعْطَاهُ الرَّايَةَ . فقال عليٌّ رضي اللَّه عنه : يا رسول اللَّه أُقاتِلُهمْ حَتَّى يَكُونُوا مِثْلَنَا ؟ فَقَالَ : « انْفُذْ عَلَى رِسلِكَ حَتَّى تَنْزِلَ بِسَاحتِهِمْ، ثُمَّ ادْعُهُمْ إِلَى الإِسْلامِ ، وَأَخْبرْهُمْ بِمَا يجِبُ مِنْ حقِّ اللَّه تَعَالَى فِيهِ ، فَواللَّه لأَنْ يَهْدِيَ اللَّه بِكَ رَجُلاً وَاحِداً خَيْرٌ لَكَ مِنْ حُمْرِ النَّعَمَ»    متفقٌ عليه


Kutoka kwa Abul-‘Abbaas Sahl bin Sa’d As-Saa’idiy (Radhi za Allah ziwe juu yake) ya kwamba Mtume ﷺ alisema siku  ya Khaybar: [Kesho nitampatia mtu bendera ambaye kwa mikono yake Mwenyezi Mungu atafungua (mji huu). Mtu huyo anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume anampenda.]  Watu wakakesha wakifikiria na kuzungumza juu ya nani atayepatiwa bendera hiyo. Kulipopambazuka watu wote walikwenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ kila mmoja anatarajia kuwa atapatiwa yeye jukumu hilo. Akasema (Mtume ﷺ): [Yuko wapi ‘Ali bin Abiy Twaalib?] Wakasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Yeye anaumwa macho.” Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu : [Mleteni kwangu.]  Akaletwa kwake, na Mtume  akampaka mate yake katika macho na kumwombea Mwenyezi Mungu . ‘Ali akapona kabisa na ugonjwa huo (wa macho) mpaka ikaonekana kama kwamba hakuwa na ugonjwa wowote na hapo akapatiwa bendera. ‘Ali (Radhi za Allah ziwe juu yake) akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nipigane nao mpaka wawe kama sisi?”  Akasema Mtume : [Endelea kwenda kwa kasi yako ya kawaida mpaka ufike katika bonde lao na hapo muweke kambi yenu. Kisha waite katika Uislamu na uwajulishe habari kuhusu yanayo wajibika kwao juu ya haki ya Mwenyezi Mungu kwao. Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu! Mwenyezi Mungu akimuongoa mtu mmoja kupitia kwako ni bora kuliko kundi la ngamia wekundu.]     [Imepokewa na Muslim]


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.