KINGA YA MUISLAMU
Mtu akisikia Muadhini anaadhini anatakiwa asema kama anavyosema Muadhini, ila atakapo sema:
“حي على الصلاة ، وحي على الفلاح”
“Hayya ala Swalaah,Hayya alal falaah”
[Njooni kwenye swala,Njoni kwenye mafanikio.]
Yeye hatomuigiza bali anatakiwa aseme:
“لا حول ولا قوة إلا بالله”
Laa Haula walaa quwwata Illaa Billah
[Hapana uwezo wala nguvu ila za Mwenyezi Mungu.] [Imepokewa na Bukhari].
Anatikiwa mtu aseme:
“وأنا أشهد أن لا إله إلا الله ، وحده لا شريك له ، وأن محمد عبده ورسوله ، رضيت بالله رباً ، وبمحمداً رسولاً وبالإسلام ديناً”
[Na mimi pia nakiri kwa moyo na kusema kwa ulimi kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki, ila Allaah Mmoja Peke Yake, hana mshirika wake na kwamba Muhammad ni mja Wake, na ni Mtume Wake. Nimeridhika kuwa Mwenyezi Mungu ndie Mola wangu, na kuwa Muhammad ni Mtume wangu, na kuwa Uislamu ndio dini yangu.] [Imepokewa na Muslim.]
[Atasema hivyo baada ya shahada ya Muadhini pale atakaposema Ash’hadu anlaa ilaha illa llah,wa Ash’hadu anna Muhammad Rasuulu llah.]
Kisha baada ya kumjibu Muadhini atamswalia Mtume ﷺ
Kisha atasema:
[اللهم رب هذه الدعوة التامة ،والصلاة القائمة، آت محمداً الوسيلة والفضيلة، وأبعثه مقاماً محموداً الذي وعدته، [ إنك لا تخلف الميعاد”]
[Ewe Mwenyezi Mungu , Bwana wa mlingano (mwito) huu uliotimia, na swala ilio simama, mpe Mtume Muhammad ﷺ Wasila, na fadhila, na mfikishe daraja yenye kusifiwa, ambayo umemuahidi.] (kwani wewe hukhalifu ahadi) [Imepokewa na Bukhari na ilioko kwe mabano imepokewa na Al-Bayhaqi na Isnadi yake ni Mzuri kama alivyo sema Ibnu Baaz katika kitabu Tuhfatul Akhyaar.]
SIKILIZA DUA ZA ADHANA