0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

157. Riyadhu Swalihina Mlango wa kuzihifadhi Sunna na Adabu zake Hadithi ya 02


BUSTANI YA WATU WEMA


رياض الصالحين 


عَنْ أَبِي نَجِيحٍ الْعِرْباضِ بْنِ سَارِيَة رضي اللَّه عنه قال : وَعَظَنَا رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم مَوْعِظَةً بليغةً وَجِلَتْ مِنْهَا الْقُلُوبُ وَذَرَفَتْ مِنْهَا الْعُيُون ، فقُلْنَا : يا رَسولَ اللَّه كَأَنَهَا موْعِظَةُ مُوَدِّعٍ فَأَوْصِنَا . قال : « أُوصِيكُمْ بِتَقْوى اللَّه، وَالسَّمْعِ وَالطَّاعَةِ وإِنْ تَأَمَّر عَلَيْكُمْ عَبْدٌ حبشيٌ ، وَأَنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ فَسَيرى اخْتِلافاً كثِيرا . فَعَلَيْكُمْ بسُنَّتي وَسُنَّةِ الْخُلُفَاءِ الرَّاشِدِينَ الْمَهْدِيِّينَ ، عضُّوا عَلَيْهَا بالنَّواجِذِ ، وإِيَّاكُمْ ومُحْدثَاتِ الأُمُورِ فَإِنَّ كُلَّ بِدْعَةٍ ضلالَةٌ »    رواه أبو داود ، والترمذِي وقال حديث حسن صحيح


Kutoka kwa Abuu Najiyh Al-‘Irbaadh bin Saariyah Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: alitupa sisi Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ mawaidha mazito (yenye maana makubwa), nyonyo zikaingia khofu na macho  yakabubujikwa na machozi. Tukamwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, inaonekana kana kwamba haya mawaidha ni yakutuaga, basi tuusie. Akasema: [Nawausia kumcha Mwenyezi Mungu, na kusikiliza na kutii, hata kama mkiongozwa na mtumwa mhabeshi. Hakika atakayeishi umri mrefu miongoni mwenu ataona khitilafu nyingi. Kwa hivyo ninyi shikamaneni na Sunna zangu na Sunna za  Makhalifa waongofu wenye kuongoza. Ishikilieni (Sunna) kwa magego. Na tahadharini mambo yenye kuzushwa,(katika Dini) hakika kila lenye kuzuliwa ni upotevu.]   [Abuu Dawud na At-Tirmidhy, na amesema: Hadithi hii ni Hasan Sahih]


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.