BUSTANI YA WATU WEMA
عنْ أَبِي محمدٍ عبدِ اللَّهِ بنِ عمرو بن العاص رضي اللَّه عنهما قال : قال رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : « أَرْبعُونَ خَصْلةً أَعلاها منِيحةُ الْعَنْزِ، ما مِنْ عامَلٍ يعملَ بِخَصْلَةٍ مِنْها رجاءَ ثَوَابِهَا وتَصْدِيقَ موْعُودِهَا إِلاَّ أَدْخلَهُ اللَّهُ بِهَا الْجنَّةَ » رواه البخارى
الْمنِيحةُ » : أَنْ يُعْطِيَهُ إِيَّاهَا ليأْكُل لبنَهَا ثُمَّ يَردَّهَا إِليْهِ»
Kutoka kwa Abuu Muhammad, ‘Abdullaah bin ‘Amruw bin ‘Aasw Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Mtume ﷺ : [Kuna mambo arubaini ya wema, la juu kabisa ni mtu akopeshe mbuzi wake. Hakuna yeyote atakayetenda mojawapo katika hayo kwa kutarajia thawabu zake na kusadikisha miadi yake, isipokuwa Mwenyezi Mungu Atamuingiza Peponi.] [Imepokewa na Bukhari]
Maniha: Ni mtu kupeana mbuzi wako ili apate kunywa maziwa yake kisha amrudishie mwenyewe.
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله