0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

137. Riyadhu Swalihina Mlango wa Ubainifu wa Njia nyingi za Kheri Hadithi ya 21


BUSTANI YA WATU WEMA


1463655589


عنْ أَبِي الْمُنْذِر أُبيِّ بنِ كَعبٍ رضي اللَّه عنه قال : كَان رجُلٌ لا أَعْلمُ رجُلا أَبْعَدَ مِنَ الْمَسْجِدِ مِنْهُ ، وكَانَ لا تُخْطِئُهُ صلاةٌ فَقِيل لَه ، أَوْ فقُلْتُ لهُ: لَوْ اشْتَريْتَ حِماراً ترْكَبُهُ في الظَّلْماءِ ، وفي الرَّمْضَاءِ فَقَالَ : ما يسُرُّنِي أَن منْزِلِي إِلَى جنْب الْمسْجِدِ ، إِنِّي أُرِيدُ أَنْ يُكْتَب لِي ممْشَايَ إِلَى الْمَسْجد ، ورُجُوعِي إِذَا رجعْتُ إِلَى أَهْلِي ، فقالَ رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : « قَدْ جمع اللَّهُ لكَ ذلِكَ كُلَّهُ »   رواه مسلم

« وفي روايةٍ : « إِنَّ لَكَ مَا احْتسَبْت

 « الرمْضَاءُ » الأَرْضُ الَّتِي أَصَابَهَا الْحرُّ الشَّديدُ


Kutoka kwa Abuu Al-Mundhir, Ubayy bin Ka’ab Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwepo mtu mmoja, sijui kama kuna mwengine aliyekuwa anaishi mbali zaidi na Msikiti kulikoni yeye, alikuwa hapitwi na Swala yoyote. Akaulizwa au nikamuuliza: Waonaje lau ungalinunua punda ukampanda wakati wa giza na wakati mchanga ukiwa umepata joto? Akajibu: Sipendelei nyumba yangu iwepo karibu na Msikiti, mimi nataka niandikiwe hatua zangu za kwenda Msikitini na kurejea kwangu kwa familia yangu.” Mtume akasema: [Mwenyezi Mungu Ameshakujumuishia yote hayo.]    [Imepokewa na Muslim]

Na katika Riwaya nyingine imesema: [Umeshapata ulilotarajia.]


 شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله



Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.