0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MLANGO WA 21 YALIKUJA KUHUSU MTUME ALIVYOHAMI TAWHIID NA KUZIBA KILA NJIA INAYOPELEKEA KWENYE SHIRK

KITAAB AT-TAWHIID

باب (21) ما جاء في حماية المصطفى صلى الله عليه وسلم جناب التوحيد وسده كل طريق يوصل إلى الشرك

وقول الله تعالى: {لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِنْ أَنْفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُمْ بِالْمُؤْمِنِينَ رَؤُوفٌ رَحِيمٌ فَإِنْ تَوَلَّوْا فَقُلْ حَسْبِيَ اللَّهُ لا إِلَهَ إِلاَّ هُوَ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَهُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ}

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: “لا تجعلوا بيوتكم قبورا، ولا تجعلوا قبري عيدا، وصلوا عليّ فإن صلاتكم تبلغني حيث كنتم”   رواه أبو داود بإسناد حسن، رواته ثقات

وعن علي بن الحسين: “أنه رأى رجلا يجيء إلى فرجة كانت عند قبر النبي صلى الله عليه وسلم فيدخل فيها فيدعو، فنهاه، وقال: ألا أحدثكم حديثا سمعته من أبي عن جدي عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: لا تتخذوا قبري عيدا، ولا بيوتكم قبورا، وصلوا علي،فإن تسليمكم يبلغني أين كنتم”   رواه في المختارة 

:فيه مسائل

الأولى:  تفسير آية براءة

الثانية: إبعاده أمته عن هذا الحمى غاية البعد

الثالثة:  ذكر حرصه علينا ورأفته ورحمته

الرابعة:  نهيه عن زيارة قبره على وجه مخصوص، مع أن زيارته من أفضل الأعمال

الخامسة:  نهيه عن الإكثار من الزيارة

السادسة:  حثه على النافلة في البيت

السابعة: أنه متقرر عندهم أنه لا يصلى في المقبرة

الثامنة: تعليله ذلك بأن صلاة الرجل وسلامه عليه يبلغه وإن بعد، فلا حاجة إلى ما يتوهمه من أراد القرب

التاسعة:  كونه صلى الله عليه وسلم في البرزخ تعرض أعمال أمته في الصلاة والسلام عليه

MLANGO WA 21 YALIKUJA KUHUSU MTUME ALIVYOHAMI TAWHIID NA KUZIBA KILA NJIA INAYOPELEKEA KWENYE SHIRK

Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Hakika amekwisha kujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe; yanamhuzunisha yanayo kutaabisheni; anakuhangaikieni sana. Kwa Waumini ni mpole na mwenye huruma.Basi wakigeuka, wewe sema: Mwenyezi Mungu ananitosheleza. Hapana mungu isipokuwa Yeye tu. Mimi namtegemea Yeye, na Yeye ndiye Mola Mlezi wa Kiti Kikuu cha Enzi.]     At-Tawba: 128-129

Imepokelewa toka kwa Abuu Hurayrah (Radhi za Allah ziwe juu yake) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ Amesema: [Msifanye nyumba zenu makaburi, wala msilifanye kaburi langu kuwa Idi (ni pahala pa kurejewa rejewa) na niswalieni, kwani kuniswalia kwenu kunanifikia popote mlipo]    [Abuu Daawuwd kwa isnaad Hasan ya wasimuliaji wanaotegemewa]

Na Imepokelewa kutoka kwa ‘Aliy bin Al-Husayn kwamba alimwona mtu akitoka kwenye upenyo uliokuwa katika ukuta wa kaburi la Mtume wa Mwenyezi Mungu akiingia na kuomba. Akamzuia akamwambia: Nikujulishe Hadithi nilioisikia kutoka kwa baba yangu kutoka kwa babu yangu kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  ﷺ amesema: [Msifanye kaburi langu kuwa ni pahala pa kurejewa rejewa, wala [msifanye] nyumba zenu makaburi, [kwa kutokuswali ndani yake] na niswalieni kwenu kuniswalia kunanifikia popote mlipo]    [Al-Mukhtaar – mkusanyo wa Hadith za Imaam Al-Maqdisiyy Al-Hanbaliyyi]

Masuala Muhimu Yaliyomo:

1. Tafsiri ya Ayah katika Suwrah Al-Baraa-ah (At-Tawbah 9:128-129)).

2. Kuwaweka mbali Ummah wake  na mipaka ya shirki kadiri iwezekanavyo.

3. Pupa lake Mtume  ﷺ juu yetu, na upole wake na huruma yake kwetu.

4. Katazo lake Mtume   juu ya kuzuru kaburi lake kwa njia fulani (isiyopasa ki shariy’ah) japo kuzuru kaburi  ni miongoni mwa ‘amali njema kabisa.

5. Makatazo ya kukithirisha mno kuzuru kaburi lake.

6. Himizo lake la kuswali Nawaafil (Swala za Sunnah) nyumbani.

7. Kukubaliana kwao (Maswahaba) kwamba kuswali makaburini imekatazwa.

8. Maelezo kwamba kumswalia Mtume  ﷺ kunamfikia hata kama mtu yuko mbali vipi. Kwa hiyo hakuna haja ya kulikuribia sana kaburi lake kama wengi wanavyodhania.

9. Mtume  ﷺ  akiwa katika maisha ya Al-Barzakh huonyeshwa ‘amali za ummah wake pamoja na swalaatu was-salaamu ‘alayhi (kumtakia rahmah na amani).

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.