0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

109 FADHILA ZA KUENEZA NA KUDHIHIRISHA MAAMKUZI YA KIISLAMU

KINGA YA MUISLAMU

قال رسول الله صلى الله عليه وسلم :” لا تدخلوا الجنة حتى تؤمنوا ، ولا تؤمنوا حتى تحابوا ، أو لا أدلكم على شيءٍ إذا فعلتموه تحاببتم

أفشوا السلام بينكم

 مسلم 1/74 وغيره

Amesema Mtume ﷺ: [Hamtaingia peponi mpaka muamini, na hamtakuwa waumini wa kweli mpaka mpendane.  Hivi niwafahamishe kitu mkikifanya mtapendana?  Salimianeni baina yenu.]    [Imepokewa na Muslim na wengineo.]

 ثلاث من جمعهن فقد جمع الإيمان : الإنصاف من نفسك ، وبذل السلام للعالم ،والإنفاق من الإقتار

 البخاري مع الفتح 1/ 82

Amesema Ammar Bin Yaasir radhi za Allah ziwe juu yake  [Mambo matatu anaeyakusanya basi amekusanya  Imani:   uadilifu wa nafsi yako, na kutowa salam kwa watu wote na kutoa (sadaka) hali ya kuwa ni mchache wa mali]        [Imepokewa na Bukhari.]

 وعن عبد الله بن عمر رضي الله عنهما : أن رجلاً سأل النبي صلى الله عليه وسلم أي الإسلام خير قال :” تطعم الطعام وتقرأ السلام على من عرفت ومن لم تعرف

البخاري مع الفتح 1/55 ومسلم 1/65

Imepokelewa kutoka kwa Abdallah bin Omar radhi za Allah ziwe juu yake  kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume ﷺ Ni uislamu gani bora?  Mtume ﷺ akamjibu, [Kulisha (maskini) na kumsalimia unaemjua na usiemjua]       [Imepokelewa na Bukhari na Muslim.]

 

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.