0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

108 FADHILA ZA KUMSWALIA MTUME ﷺ

KINGA YA MUISLAMU

” قال صلى الله عليه وسلم ” من صلى علي صلاة صلى الله عليه بها عشراً

 أخرجه مسلم 1/288

Amesema Mtume ﷺ [Yoyote atakaeniswalia mimi mara moja basi Mwenyezi Mungu atamswalia mara kumi.]         [Imepokewa na Bukhari.]

[ وقال صلى الله عليه وسلم : [ لا تجعلوا قبري عيداً وصلوا علي ؛ فإن صلاتكم تبلغني حيث كنتم

أبو داود 2/218 وأحمد 2/367 وصححه الألباني

Na amesema Mtume ﷺ: [Musilifanye kaburi langu kuwa ni Idi (mahali pa kufanya ibada inayorejewa ) na niswalieni kwani kuniswalia kwenu kunanifikia popote mulipo.]     [Imepokewa na Abuu Daud na Ahmad na kusahihishwa na Al-Baaniy.]

[ وقال صلى الله عليه وسلم : [ البخيل من ذكرت عندهُ فلم يصل علي

الترمذي 5/551 وغيره

Pia amesema Mtume ﷺ [Bakhili ni yule ambaye nikitajwa haniswalii.]     [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy.]

[ وقال صلى الله عليه وسلم [ إن لله ملائكة سياحين في الأرض يبلغوني من أمتي السلام

النسائي ،والحاكم 2/421 وصححه الألباني

Na amesema Mtume ﷺ: [Hakika Mwenyezi Mungu ana malaika wanamzunguka katika ardhi, wananiletea salamu kutoka kwa ummah wangu.]      [Imepokewa na Al-Nnasaai na Al-Haakim na kusahihishwa na Al-Baaniy.]

[ وقال صلى الله عليه وسلم [ ما من أحد يسلم علي إلا رد الله على روحي حتى أروُدَّ عليه السلام

أبو داود برقم 2041

Na pia akasema Mtume ﷺ: [Hakuna mtu yoyote anaeniswalia ila Mwenyezi Mungu hunirudisha roho yangu ili nimrudishie salamu.]      [Imepokewa na Abuu Daud.]

SIKILIZA DUA HII 

  

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.