KINGA YA MUISLAMU
Imepokelewa kutoka kwa Ibn Omar radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume ﷺ alikuwa akirudi vitani au kutoka Hijjah katika kila akipanda mlima akisema:
[ اللهُ أَكْـبَر، اللهُ أَكْـبَر، اللهُ أَكْـبَر ]
[Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa]
Kisha akisema:
لا إله إلا الله وحده لا شريك لهُ ،لهُ الملك ، ولهُ الحمدُ وهو على كل شيءٍ قدير ، آيبون ،تائبون ، عابدون ، لربنا حامدون ،صدق الله وعده،ونصر عبده،وهزم الأحزاب وحده
[Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, hali ya kuwa peke yake, wala hana mshirika. Ufalme ni wake, na sifa njema ni zake, na Yeye juu ya kila kitu ni mueza, tunarudi hali ya kuwa tunatubia, tunaabudu, na Mola wetu tunamsifu, amesadikisha Mwenyezi Mungu ahadi yake, na amemnusuru mja wake, na amevishinda vikosi peke yake.] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
DUA YA MSAFIRI AKIRUDI KUTOKA SAFARINI