0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

07. MLANGO WA YAKINI NA KUMTEGEMEA MWENYEZI MUNGU

BUSTANI YA WATU WEMA


     قال اللَّه تعالى : {وَلَمَّا رَأَى الْمُؤْمِنُونَ الْأَحْزَابَ قَالُوا هَٰذَا مَا وَعَدَنَا اللَّهُ وَرَسُولُهُ وَصَدَقَ اللَّهُ وَرَسُولُهُ ۚ وَمَا زَادَهُمْ إِلَّا إِيمَانًا وَتَسْلِيمًا}       الأحزاب:22

وقال تعالى :{الَّذِينَ قَالَ لَهُمُ النَّاسُ إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُوا لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَانًا وَقَالُوا حَسْبُنَا اللَّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ فَانقَلَبُوا بِنِعْمَةٍ مِّنَ اللَّهِ وَفَضْلٍ لَّمْ يَمْسَسْهُمْ سُوءٌ وَاتَّبَعُوا رِضْوَانَ اللَّهِ ۗ وَاللَّهُ ذُو فَضْلٍ عَظِيمٍ}    آل عمران: 174-173

وقال اللَّه تعالى : {وَتَوَكَّلْ عَلَى الْحَيِّ الَّذِي لَا يَمُوتُ}   الفرقان:58

وقال تعالى : {وَعَلَى اللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ}   التوبة:51

وقال تعالى : {فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ ۚ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُتَوَكِّلِينَ}   آل عمران:159

والآيات في الأمر بالتوكل كثيرة معلومة

          وقال تعالى : {وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ فَهُوَ حَسْبُهُ } : أي كافيه

{وقال تعالى : {إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ

والآيات في فضل التوكل كثيرة معروفة


Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Na Waumini walipo yaona makundi, walisema: Haya ndiyo aliyo tuahidi Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamesema kweli. Na hayo hayakuwazidisha ila Imani na ut’iifu.]     [Al-Ah’zab:22]

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Walio ambiwa na watu: Kuna watu wamekukusanyikieni, waogopeni! Hayo yakawazidishia Imani, wakasema: Mwenyezi Mungu anatutosha, naye ni mbora wa kutegemewaBasi wakarudi na neema na fadhila za Mwenyezi Mungu. Hapana baya lilio wagusa, na wakafuata yanayo mridhi Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kuu.]      [Suurat Al ‘Imran:173-174]

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Na mtegemee Aliye Hai, ambaye hafi.]    [Surat Al-Furqan:58]

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu!]    [Suuratut Tawba:51]

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Na ukisha kata shauri basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao mtegemea.]    [Suurat Al ‘Imran:159]

Na Aya zinazo amrisha kumtegemea Menyezi Mungu ni nyini na zajulikana.

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Na anaye mtegemea Mwenyezi Mungu Yeye humtosha]  [Suuratul Att’alaaq:3]

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Hakika Waumini ni wale ambao anapo tajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hujaa khofu, na wanapo somewa Aya zake huwazidisha Imani, na wakamtegemea Mola wao Mlezi.] [Suurat Al Anfaal:2]

Na Aya katika Fadhla ya Kumtegemea Mwenyezi Mungu ni nyini na zajulikana.


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.