BUSTANI YA WATU WEMA
عن ابنِ عبَّاسٍ ، رضيَ اللَّه عنهمَا ، قال : « كُنْتُ خَلْفَ النَّبِيِّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يوْماً فَقال : « يَا غُلامُ إِنِّي أُعلِّمكَ كَلِمَاتٍ : « احْفَظِ اللَّهَ يَحْفَظْكَ احْفَظِ اللَّهَ تَجِدْهُ تُجَاهَكَ ، إِذَا سَأَلْتَ فَاسْأَل اللَّه ، وَإِذَا اسْتَعَنْتَ فَاسْتَعِنْ بِاللَّهِ ، واعلَمْ : أَنَّ الأُمَّةَ لَو اجتَمعتْ عَلَى أَنْ ينْفعُوكَ بِشيْءٍ ، لَمْ يَنْفعُوكَ إِلاَّ بِشَيْءٍ قَد كَتَبَهُ اللَّهُ لَكَ ، وإِنِ اجْتَمَعُوا عَلَى أَنْ يَضُرُّوك بِشَيْءٍ ، لَمْ يَضُرُّوكَ إِلاَّ بَشَيْءٍ قد كَتَبَهُ اللَّه عليْكَ ، رُفِعَتِ الأقْلامُ ، وجَفَّتِ الصُّحُفُ
رواهُ التِّرمذيُّ وقَالَ : حديثٌ حسنٌ صَحيحٌ
وفي رواية غيرِ التِّرْمِذيِّ : « احفظَ اللَّهَ تَجِدْهُ أَمَامَكَ ، تَعَرَّفْ إِلَى اللَّهِ في الرَّخَاءِ يعرِفْكَ في الشِّدةِ ، واعْلَمْ أَنّ مَا أَخْطَأَكَ لَمْ يَكُنْ لِيُصيبَك ، وَمَا أَصَابَكَ لمْ يَكُن لِيُخْطِئَكَ واعْلَمْ أنّ النَّصْرَ مَعَ الصَّبْرِ ، وأَنَّ الْفَرَجَ مَعَ الْكَرْب ، وأَنَّ مَعَ الْعُسرِ يُسْراً
Kutoka kwa Ibnu ‘Abbaas Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Siku moja nilikuwa nyuma ya Mtume wa Mungu ﷺ (juu ya mnyama). Akaniambia: [Ewe kijana, mimi nitakufundisha maneno: Mhifadhi Mwenyezi Mungu Naye Atakuhifadhi. Mhifadhi Mwenyezi Mungu utamkuta yupo mbele yako. Unapoomba, muombe Mwenyezi Mungu. Unapotaka msaada, mtake msaada Mwenyezi Mungu. Fahamu kuwa, lau ummah (wote) utajikusanya ili wakunufaishe kwa jambo, basi hawataweza kukunufaisha ila kwa jambo Alilokuandikia Mwenyezi Mungu; na wakijikusanya ili wakudhuru kwa jambo, hawataweza kukudhuru ila kwa jambo Alilokuandikia Mwenyezi Mungu. Kalamu zimeshainuliwa na karatasi zimeshakauka.] [Imepokewa na At-Tirmidhiy, na amesema: Hadiyth hii ni Hasan Sahih]
Na katika Riwaya nyingine isiyokuwa ya At-Tirmidhiy imesema:
[Mhifadhi Mwenyezi Mungu utamkuta Yupo mbele yako. Mjue Mwenyezi Mungu katika raha naye Atakujua katika shida. Ujue kuwa, lililokukosa halikuwa ni lenye kukupata, na lililokusibu halikuwa ni lenye kukukosa. Ujue kuwa Nusra ipo pamoja na Subira, faraja ipo pamoja na dhiki, na kwenye uzito kuna wepesi.]
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله