0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

060. Riyadhu Swalihina Mlango wa Kumchunga Mungu Hadithi ya 01


BUSTANI YA WATU WEMA


رياض الصالحين


عَنْ عُمرَ بنِ الخطابِ ، رضيَ اللَّهُ عنه ، قال: «بَيْنما نَحْنُ جُلُوسٌ عِنْد رسولِ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، ذَات يَوْمٍ إِذْ طَلع عَلَيْنَا رجُلٌ شَديدُ بياضِ الثِّيابِ ، شديدُ سوادِ الشَّعْر ، لا يُرَى عليْهِ أَثَر السَّفَرِ ، ولا يَعْرِفُهُ منَّا أَحدٌ ، حتَّى جَلَسَ إِلَى النَّبِيِّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، فَأَسْنَدَ رَكْبَتَيْهِ إِلَى رُكبَتيْهِ ، وَوَضع كفَّيْه عَلَى فخِذيهِ وقال : يا محمَّدُ أَخبِرْنِي عن الإسلام فقالَ رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : الإِسلامُ أَنْ تَشْهَدَ أَنْ لا إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ ، وأَنَّ مُحَمَّداً رسولُ اللَّهِ وَتُقِيمَ الصَّلاَةَ ، وَتُؤتِيَ الزَّكاةَ ، وتصُومَ رَمضَانَ ، وتحُجَّ الْبيْتَ إِنِ استَطَعتَ إِلَيْهِ سَبيلاً
قال : صدَقتَ . فَعجِبْنا لَهُ يسْأَلُهُ ويصدِّقُهُ ، قَالَ : فَأَخْبِرْنِي عن الإِيمانِ . قَالَ: أَنْ تُؤْمِن بِاللَّهِ وملائِكَتِهِ ، وكُتُبِهِ ورُسُلِهِ ، والْيومِ الآخِرِ ، وتُؤمِنَ بالْقَدَرِ خَيْرِهِ وشَرِّهِ . قال: صدقْتَ قال : فأَخْبِرْنِي عن الإِحْسانِ . قال : أَنْ تَعْبُدَ اللَّه كَأَنَّكَ تَراهُ . فإِنْ لَمْ تَكُنْ تَراهُ فإِنَّهُ يَراكَ قَالَ : فَأَخْبِرْنِي عن السَّاعةِ . قَالَ : مَا المسْؤُولُ عَنْهَا بأَعْلَمَ مِن السَّائِلِ . قَالَ : فَأَخْبرْنِي عَنْ أَمَاراتِهَا . قَالَ أَنْ تلدَ الأَمَةُ ربَّتَها ، وَأَنْ تَرى الحُفَاةَ الْعُراةَ الْعالَةَ رِعاءَ الشَّاءِ يتَطاولُون في الْبُنيانِ ثُمَّ انْطلَقَ ، فلبثْتُ ملِيًّا ، ثُمَّ قَالَ : يا عُمرُ ، أَتَدرِي منِ السَّائِلُ قلتُ : اللَّهُ ورسُولُهُ أَعْلمُ قَالَ : فَإِنَّهُ جِبْرِيلُ أَتَاكُمْ يُعلِّمُكم دِينِكُمْ »       رواه مسلمٌ


Kutoka kwa Umar bin Al-Khattwaab Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Siku moja tulikuwa tumekaa mbele ya Mtume ﷺ, kwa ghafla akatutokea mtu mmoja ambaye nguo zake zilikuwa nyeupe pepe na nywele zake zilikuwa nyeusi sana; hakuwa na alama ya machofu ya safari na wala hapakuwa na hata mmoja katika sisi anaemjua. Alienda akakaa karibu na Mtume  akayategemeza magoti yake karibu na magoti yake (Mtume ) na akaweka viganja vyake juu ya mapaja yake kisha akasema; Ewe Muhammad! Nieleze kuhusu Uislaamu.  Mtume  akasema:  [Uislamu ni kukiri kuwa hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na Muhammad ni Mtume wa Mungu, kusimamisha Swala, kutoa Zaka, na kufunga Mwezi wa Ramadhani na kwenda kuhiji (Makkah) ukiweza.] Akasema  “Umesema kweli.” Tukamstaajabia anamuliza na Kumsadikisha. Na akauliza (tena): Nieleze kuhusu Imani.  Akasema: [Ni kumwamini Mungu ,na  Malaika Wake,na Vitabu Vyake, na Mitume yake na siku ya Mwisho, na  kuamini Qadari  (majaaliwa ya Allaah) ya kheri zake na shari zake.] Akasema : “Umesema kweli.”. Akasema: “Hebu nielezee kuhusu Ihsaan.”  Akasema Mtume : [Ni kumuabudu Mwenyezi Mungu kama vile unamuona na kama humuoni basi Yeye Anakuona.]  Akasema : “Niambie kuhusu Qiyama.”  Akajibu: [Anayeulizwa si mjuzi kama kuliko anayeuliza.] akamwambia: “Nijulishe alama zake.”: Akajibu (Mtume ): [Mjakazi atakapo mzaa Bwana wake, na utaona wanaotembea bila ya viatu, wenda uchi, mafukara wachunga Mbuzi wakishindana kujenga majumba marefu.] alafu yule bwana akaenda zake,na nilitulia kidogo. Kisha Mtume ﷺ : “Ewe ‘Umar! Je, unamjua ni nani yule aliyekuwa akiuliza? Nikasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanajua zaidi.  Akasema Mtume : [Huyu ni Jibril, alikuja kuwafundisha dini yenu.]    [Imepokewa na Muslim]


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله





Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.