0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

058. Riyadhu Swalihina Mlango wa Ukweli Hadithi ya 05

BUSTANI YA WATU WEMA


عَنْ أبي هُريْرة رضي اللَّهُ عنه قال : قال رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم: « غزا نَبِيٌّ مِنَ الأَنْبِياءِ صلواتُ اللَّه وسلامُهُ علَيهِمْ فَقَالَ لقوْمِهِ : لا يتْبعْني رَجُلٌ ملَكَ بُضْعَ امْرَأَةٍ. وَهُوَ يُرِيدُ أَن يَبْنِيَ بِهَا وَلَمَّا يَبْنِ بِها ، ولا أَحدٌ بنَى بيُوتاً لَمْ يرفَع سُقوفَهَا ، ولا أَحَدٌ اشْتَرى غَنَماً أَوْ خَلَفَاتٍ وهُو يَنْتَظرُ أوْلادَهَا . فَغزَا فَدنَا مِنَ الْقَرْيةِ صلاةَ الْعصْرِ أَوْ قَريباً مِنْ ذلكَ ، فَقَال للشَّمس : إِنَّكِ مَأمُورةٌ وأَنا مأمُورٌ ، اللهمَّ احْبسْهَا علَينا ، فَحُبستْ حَتَّى فَتَحَ اللَّهُ عليْهِ ، فَجَمَعَ الْغَنَائِم ، فَجاءَتْ  يَعْنِي النَّارَ لتَأكُلهَا فَلَمْ تطْعمْهَا ، فقال: إِنَّ فِيكُمْ غُلُولاً، فليبايعنِي منْ كُلِّ  قبِيلَةٍ رجُلٌ ، فلِزقتْ يدُ رَجُلٍ بِيدِهِ فَقَالَ : فِيكُم الْغُلولُ ، فليبايعنِي قبيلَتُك ، فلزقَتْ يدُ رجُليْنِ أو ثلاثَةٍ بِيَدِهِ فقَالَ : فِيكُمُ الْغُلُولُ ، فَجاءوا برَأْسٍ مِثْلِ رَأْس بَقَرَةٍ مِنْ الذَّهبِ ، فوضَعها فَجَاءَت النَّارُ فَأَكَلَتها ، فلمْ تَحل الْغَنَائِمُ لأحدٍ قَبلَنَا ، ثُمَّ أَحَلَّ اللَّهُ لَنا الغَنَائِمَ لمَّا رأَى ضَعفَنَا وعجزنَا فأحلَّها لنَا »      متفقٌ عليه


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Kutoka kwa Abuu Hurayrah Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesmea Mtume wa Mungu : [Kuna Nabiy mmoja alitaka kwenda kupigana jihadi, akawaambia watu yake: “Asinifuate Yeyote aliyeoa na yeye yuwataka kumuingilia kwake lakini bado hajamuingia, au yule aliyejenga kuta za nyumba lakini hajati paa, au yule aliyenunua mbuzi au ngami wenye mimba anangojea wazae, (akaenda na mujaahidina wake katika mji aliokusudia.) Akavamia (kijiji) Alipofika hapo karibu na mji karibu na Swala ya Alasiri,au karibu ya alasiri aliliambia jua: “Hakika wewe umeamrishwa (na Mungu) na mimi nimeamrishwa, Ewe Mola, lizuie kwa ajili yetu.” Likazuiliwa mpaka Mwenyezi Mungu Alipompa ushindi. Akazikusanya ghanima, moto ukaja ili upate kuziteketeza, lakini haukuweza kuziteketeza. Akawaambia: “Hakika kati yenu kuna aliyefanya khiyana, kwa hiyo katika kila kabila anbai (afunge kiapo cha ahadi) mtu mmoja.” Mkono wa mtu mmoja ukanata katika mkono wake. Akawaambia: “Kwenu kuna khiyana, kwa hivyo kabila lako lote linibai” Mikono ya watu wawili au watatu ikanata kwenye mkono wake.” Akawaambia: “Kwenu kuna khiyana,” Wakaleta dhahabu mfano wa kichwa cha ng’ombe. Yule Nabiy akaiweka, moto ukaja na ukaiteketeza. Ghanima haikuhalalishwa kwa yoyote kabla yetu. Kisha Mwenyezi Mungu Akatuhalalishia ghanima Alipoona udhaifu wetu na ajizi yetu (na kukosa hila), Akatuhalalishia.]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim]


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.