0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

044. Riyadhu Swalihina Mlango wa Subira Hadithi ya 20


BUSTANI YA WATU WEMA


رياض الصالحين


وعنْ أَنَسٍ رضي اللَّه عنه قال : كَانَ ابْنٌ لأبي طلْحةَ رضي اللَّه عنه يَشْتَكي ، فخرج أبُو طَلْحة ، فَقُبِضَ الصَّبِيُّ ، فَلَمَّا رَجَعَ أَبُو طَلْحةَ قال : ما فَعَلَ ابنِي ؟ قَالَت أُمُّ سُلَيْم وَهِيَ أُمُّ الصَّبيِّ : هو أَسْكَنُ مَا كَانَ ، فَقَرَّبَتْ إِلَيْهِ الْعَشَاءَ فَتَعَشَّى ، ثُمَّ أَصَابَ مِنْهَا، فَلَمَّا فرغَ قَالَتْ : وارُوا الصَّبيَّ فَلَمَّا أَصْبحَ أَبُو طَلْحَة أَتَى رسولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم فَأَخْبرهُ، فَقَالَ: « أَعرَّسْتُمُ اللَّيْلَةَ ؟ قَالَ : نَعَمْ ، قال : « اللَّهمَّ باركْ لَهُما » فَولَدتْ غُلاماً فقَالَ لِي أَبُو طَلْحَةَ : احْمِلْهُ حتَّى تَأَتِيَ بِهِ النبيَّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، وبَعثَ مَعهُ بِتمْرَات ، فقال : «أَمعهُ شْيءٌ ؟ » قال : نعمْ ، تَمراتٌ فَأَخَذَهَا النَّبِيُّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم فَمضَغَهَا ، ثُمَّ أَخذَهَا مِنْ فِيهِ فَجَعَلَهَا في في الصَّبيِّ ثُمَّ حَنَّكَه وسمَّاهُ عبدَ اللَّهِ متفقٌ عليه
وفي روايةٍ للْبُخَاريِّ : قال ابْنُ عُيَيْنَة : فَقَالَ رجُلٌ منَ الأَنْصارِ : فَرَأَيْتُ تَسعة أَوْلادٍ كلُّهُمْ قدْ قَرؤُوا الْقُرْآنَ ، يعْنِي مِنْ أَوْلادِ عَبْدِ اللَّه الْموْلُود
وفي روايةٍ لمسلِم : ماتَ ابْنٌ لأبِي طَلْحَةَ مِنْ أُمِّ سُلَيْمٍ ، فَقَالَتْ لأهْلِهَا : لا تُحَدِّثُوا أَبَا طَلْحَةَ بابنِهِ حتَّى أَكُونَ أَنَا أُحَدِّثُهُ ، فَجَاءَ فَقَرَّبَتْ إِلَيْهِ عَشَاءً فَأَكَلَ وشَرِبَ ، ثُمَّ تَصنَّعتْ لهُ أَحْسنَ ما كانتْ تَصَنَّعُ قَبْلَ ذلكَ ، فَوقَعَ بِهَا ، فَلَمَّا أَنْ رأَتْ أَنَّهُ قَدْ شَبِعِ وأَصَابَ مِنْها قَالتْ: يا أَبَا طلْحةَ ، أَرَايْتَ لَوْ أَنَّ قَوْماً أَعارُوا عارِيتهُمْ أَهْل بيْتٍ فَطَلبوا عاريَتَهُم ، ألَهُمْ أَنْ يمْنَعُوهَا؟ قَالَ : لا ، فَقَالَتْ : فاحتسِبْ ابْنَكَ . قَالَ : فغَضِبَ ، ثُمَّ قَالَ : تركتنِي حتَّى إِذَا تَلطَّخْتُ ثُمَّ أَخْبرتِني بِابْني ، فَانْطَلَقَ حتَّى أَتَى رسولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم فأخْبَرهُ بما كَانَ ، فَقَالَ رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : « بَاركَ اللَّه لكُما في ليْلتِكُما
قال : فحملَتْ ، قال : وكَانَ رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم في سفَرٍ وهِي مَعَهُ وكَانَ رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم إِذَا أَتَى الْمَدِينَةِ مِنْ سَفَرٍ لاَ يَطْرُقُها طُرُوقاً فَدنَوْا مِنَ الْمَدِينَةِ ، فَضَرَبَهَا الْمَخاضُ ، فَاحْتَبَس عَلَيْهَا أَبُو طلْحَةَ ، وانْطلَقَ رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم . قَالَ : يقُولُ أَبُو طَلْحةَ إِنَّكَ لتعلمُ يَا ربِّ أَنَّهُ يعْجبُنِي أَنْ أَخْرُجَ معَ رسولِ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم إِذَا خَرَجَ ، وأَدْخُلَ مَعهُ إِذَا دَخَلَ ، وقَدِ احْتَبَسْتُ بِما تَرى . تقولُ أُمُّ سُلَيْمٍ : يا أَبَا طلْحةَ مَا أَجِد الَّذي كنْتُ أَجِدُ ، انْطَلِقْ ، فانْطَلقْنَا ، وضَربهَا المَخاضُ حينَ قَدِمَا فَولَدتْ غُلاماً . فقالَتْ لِي أُمِّي : يا أَنَسُ لا يُرْضِعُهُ أَحدٌ تَغْدُوَ بِهِ عَلَى رسُول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، فلمَّا أَصْبحَ احتملْتُهُ فانطَلقْتُ بِهِ إِلَى رسولِ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم . وذَكَرَ تمامَ الْحَدِيثِ


1شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



2شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Kutoka kwa Anas Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: “Alikuwa mtoto wa Abuu Twalhah akiugua. Abuu Twalahah akapata safari na kusafiri. Yule mtoto akafariki. Abuu Twalhah aliporudi”, aliuliza: “Vipi hali ya mwanangu?” Ummu Sulaym (mama wa mtoto) akamwambia: “Ametulia zaidi ya alivyokuwa.” Akampelekea chakula cha jioni akala, kisha akalala na mkewe (akamjamii). Alipomaliza, Ummu Sulaym akamwambi: “Kamzikeni mtoto.” Abuu Twalhah alipopambaukiwa, alikwenda moja kwa moja mpaka kwa Mtume ﷺ akamueleza yaliyotokea. Akamuuliza: [Usiku mlifanya tendo la ndoa?] Akajibu: “Ndiyo” Akaomba: “Ewe Mola, Wabarikie.” Akazaa mvulana. Abuu Twalhah akaniambia: “Mbebe na umepeleke kwa Mtume  akapeleka na tende kadhaa. Akauliza: “Ana kitu?” Akajibu: “Ndiyo, tende kadhaa.” Mtume  akazichua na kuzitafuna, kisha akachukua zile tende zilizokuwa kinywani mwake akazitia kwenye kinywa cha mtoto, halafu akamsugua na kumpa jina la ’Abdullaah”.   [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Na katika Riwaya nyingine ya Bukhariy imesema: “Ibnu Uyaynah amesema: “Mtu mmoja katika Answaariy akasema: “Nikawaona watoto tisa, wote wamehifadhi Qur’ani.” Yaani watoto wa ‘Abdullaah huyu aliezaliwa.

NA Riwaya nyingine ya Muslim imesema: “Abuu Twalhah alifiwa na mtoto aliyezaa naye kwa Ummu Sulaym akawaambia jamaa zake: “Msimueleze Abuu Twalhah habari ya mwanawe mpaka mimi niwe ndiye nitakaemueleza.” Akaja, akampelekea chakula jioni, akala na akanywa, halafu akajipamba kulikoni alivyojipamba siku zote. Akamjamii. Ummu Sulaym alipoona kuwa Abuu Twalhah ameshiba na amemjamii, alimwambia: “Ewe Abuu Twalhah niambie lau watu wameazima kitu kwa watu fulani kisha hao watu wakataka kitu cha kilichoazimwa, je, wao wanahaki ya kuwanyima?” Akajibu: “Hapana.” Akamwambia: Basi taraji thawabu kwa msiba wa mwanao.” Abuu Twalhah akakasirika, na akasema: “Umeniwacha mpaka nimejichafua (kwa tendo la ndoa) halafu unaniambia habari ya mwanangu?” Akaenda kwa Mtume   akamueleza mambo yalivyokuwa. Mtume  akawaombea [Allaah Awabarikie katika usiku wenu.] Ummu Sulaym akabeba ujauzito. Mtume  alikuwa safarini pamoja na Ummu Sulaym. Mtume ﷺ alikuwa anapowasili Madina akitoka safari, alikuwa haingii usiku. Walipowasili Madina Ummu Sulaym alianza kuhisi uchungu wa uzazi, Abuu Twalhah alibaki nyuma, Mtume  akaendelea na safari. Abuu Twalhah akasema: “Ewe Mola, hakika Unajua ya kuwa mimi hufurahishwa kusafiri pamoja na Mtume ﷺ anaposafiri, na hupenda kurudi pamoja nae anaporudi, na nimezuilika kama Uonavyo.” Ummu Sulaym akasema: “Ewe Abuu Twalhah sisikii uchungu tena niliousikia, tuondoke.” Tukaondoka. Akapatwa na uchungu tena wa kuzaa tulipokuwa tumeshawasili Madiynah, akajifungua mtoto wa kiume. Mama yangu akaniambia: “Ee Anas, mtoto huyu asinyonyeshwe na yoyote mpaka uende nae kwa Mtume .” Kulipopambauka, nilimbeba na kwenda nae kwa Mtume  …” Akaendelea mpaka mwisho wa Hadiyth.


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.