BUSTANI YA WATU WEMA
وعن أنس رضي اللَّه عنه قال : قال رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : « إِذَا أَرَادَ اللَّهُ بعبْدِهِ خَيْراً عجَّلَ لَهُ الْعُقُوبةَ في الدُّنْيَا ، وإِذَا أَرَادَ اللَّه بِعبدِهِ الشَّرَّ أمسَكَ عنْهُ بذَنْبِهِ حتَّى يُوافِيَ بهِ يَومَ الْقِيامةِ
وقَالَ النبِيُّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : « إِنَّ عِظَمَ الْجزاءِ مَعَ عِظَمِ الْبلاءِ ، وإِنَّ اللَّه تعالى إِذَا أَحَبَّ قَوماً ابتلاهُمْ ، فَمنْ رضِيَ فلَهُ الرضَا ، ومَنْ سَخِطَ فَلَهُ السُّخْطُ » رواه الترمذي وقَالَ: حديثٌ حسنٌ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Kutoka kwa Anas Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ: [Mwenyezi Mungu Anapompendea mja Wake kheri , Humuharakishia adhabu duniani. Na anapomtakia shari mja Wake, Huzuia dhambi zake ili Amlipe siku ya Qiyama.]
Na amesema Mtume ﷺ: [Malipo makubwa yapo pamoja na mitihani kubwa. Hakika Mwenyezi Mungu Anapowapenda watu, Huwapa mitihani; atakayeridhika, basi atapata Radhi (za Mwenyezi Mungu), na atakayechukia, atapata Hasira (za Mwenyezi Mungu).] [Imepokewa na At-Tirmidhiy, na amesema Hadithi hii ni Hassan]