0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

022. Riyadhu Swalihina Mlango wa Tawba Hadithi ya 10


BUSTANI YA WATU WEMA


وَعَنْ أبي نُجَيْد بِضَم النُّونِ وَفَتْح الْجيِمِ  عِمْرانَ بْنِ الحُصيْنِ الخُزاعيِّ رَضِي اللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ امْرأَةً مِنْ جُهينةَ أَتَت رَسُولَ الله صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم وَهِيَ حُبْلَى مِنَ الزِّنَا ، فقَالَتْ : يَا رسول الله أَصَبْتُ حَدّاً فأَقِمْهُ عَلَيَّ ، فَدَعَا نَبِيُّ الله صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم وَليَّهَا فَقَالَ : أَحْسِنْ إِليْهَا ، فَإِذَا وَضَعَتْ فَأْتِنِي فَفَعَلَ فَأَمَرَ بِهَا نَبِيُّ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، فَشُدَّتْ عَلَيْهَا ثِيَابُها ، ثُمَّ أَمَرَ بِهَا فرُجِمتْ ، ثُمَّ صلَّى عَلَيْهَا . فَقَالَ لَهُ عُمَرُ : تُصَلِّي عَلَيْهَا يَا رَسُولَ اللَّهِ وَقَدْ زَنَتْ ، قَالَ : لَقَدْ تَابَتْ تَوْبةً لَوْ قُسِمَتْ بَيْن سبْعِينَ مِنْ أَهْلِ المدِينَةِ لوسعتهُمْ وَهَلْ وَجَدْتَ أَفْضَلَ مِنْ أَنْ جَادَتْ بِنفْسهَا للَّهِ

عَزَّ وجَل؟،»   رواه مسلم


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله



Kutoka kwa Abuu Nujayd, ‘Imraan bin Huswayn Al-Khuza’iy Radhi za Allah ziwe juu yake amehadithia kwamba: Mwanamke kutoka kabila la Juhaynah alimuendea Mtume wa Mwenyezi Mungu naye ana mimba ya zinaa, akamwambia: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu , nimetenda dhambi inayopaswa haddi (adhabu), kwa hiyo nipitishie.” Mtume wa Mwenyezi Mungu  akamwita msimamizi wake, akamwambia: [Mfanyie ihsaan atakapojifungua basi mlete.] Yule msimamizi akafanya kama alivyoamrishwa, halafu akaja naye. Mtume wa Mwenyezi Mungu  akaamuru, akafungwe kwa nguo zake, halafu akaamuru apigwe mawe, kisha akamswalia. ‘Umar akamwambia: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, unamswalia na hali alikuwa amezini?” (Mtume ) Akamwambia: [Kwa yakini ametubia Tawba ambayo lau ingeligawanya kwa watu sabini miongoni mwa watu wa Madina, ingewatosha. Je, ushawahi kuona lililo bora kuliko yeye kujileta mwenyewe kwa Mwenyezi Mungu ﷻ?]      [Imepokewa na Muslim]


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.