0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

02. Sahih Al-Bukhari Mlango wa Mwanzo wa Ufunuo (Wahyi)


صحيح البخاري


 كتاب بَدْءِ الوَحْيِ

باب كَيْفَ كَانَ بَدْءُ الْوَحْىِ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم


حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يُوسُفَ، قَالَ: أَخْبَرَنَا مَالِكٌ، عَنْ هِشَامِ بْنِ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنِينَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا، أَنَّ الحَارِثَ بْنَ هِشَامٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ سَأَلَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، كَيْفَ يَأْتِيكَ الوَحْيُ؟ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَحْيَانًا يَأْتِينِي مِثْلَ صَلْصَلَةِ الجَرَسِ، وَهُوَ أَشَدُّهُ عَلَيَّ، فَيُفْصَمُ عَنِّي وَقَدْ وَعَيْتُ عَنْهُ مَا قَالَ، وَأَحْيَانًا يَتَمَثَّلُ لِيَ المَلَكُ رَجُلًا فَيُكَلِّمُنِي فَأَعِي مَا يَقُولُ» – قَالَتْ عَائِشَةُ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا: وَلَقَدْ رَأَيْتُهُ يَنْزِلُ عَلَيْهِ الوَحْيُ فِي اليَوْمِ الشَّدِيدِ البَرْدِ، فَيَفْصِمُ عَنْهُ وَإِنَّ جَبِينَهُ لَيَتَفَصَّدُ عَرَقًا


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ مُحَمّد بن صَالِح العُثَيْمِين رحمه الله تعالى



Sahih Al-Bukhari


Mlango wa Mwanzo wa Ufunuo (Wahyi)


Imepokewa kutoka kwa Âisha Radhi za Allah ziwe juu yake amehadithia, al-Hârith bin Hishâm Radhi za Allah ziwe juu yake alimwuliza Mtume ﷺ : “Wahyi hukujia vipi?” Mtume ﷺ akamjibu: “Wakati mwingine hunijia mfano wa mlio wa kengele, nao ndio mzito zaidi kwangu, halafu huniondokea nami nimeshayahifadhi aliyosema. Na wakati mwingine, Malaika hunijia kwa sura za mtu; akanizungumzisha, nikayahifadhi aliyosema.” ‘Aisha Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: “Kwa yakini nimemuona (Mtume) akiteremkiwa na Wahyi siku ya baridi kali, basi ukimuondokea na huku kipaji chake chamiminika jasho.


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.