0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

03. Sahih Al-Bukhari Mlango Wa Mwanzo Wa Ufunuo (Wahyi)


صحيح البخاري


 كتاب بَدْءِ الوَحْيِ

باب كَيْفَ كَانَ بَدْءُ الْوَحْىِ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم


حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ بُكَيْرٍ، قَالَ: حَدَّثَنَا اللَّيْثُ، عَنْ عُقَيْلٍ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ عُرْوَةَ بْنِ الزُّبَيْرِ، عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنِينَ أَنَّهَا قَالَتْ: أَوَّلُ مَا بُدِئَ بِهِ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنَ الوَحْيِ الرُّؤْيَا الصَّالِحَةُ فِي النَّوْمِ، فَكَانَ لاَ يَرَى رُؤْيَا إِلَّا جَاءَتْ مِثْلَ فَلَقِ الصُّبْحِ، ثُمَّ حُبِّبَ إِلَيْهِ الخَلاَءُ، وَكَانَ يَخْلُو بِغَارِ حِرَاءٍ فَيَتَحَنَّثُ فِيهِ – وَهُوَ التَّعَبُّدُ – اللَّيَالِيَ ذَوَاتِ العَدَدِ قَبْلَ أَنْ يَنْزِعَ إِلَى أَهْلِهِ، وَيَتَزَوَّدُ لِذَلِكَ، ثُمَّ يَرْجِعُ إِلَى خَدِيجَةَ فَيَتَزَوَّدُ لِمِثْلِهَا، حَتَّى جَاءَهُ الحَقُّ وَهُوَ فِي غَارِ حِرَاءٍ، فَجَاءَهُ المَلَكُ فَقَالَ: §اقْرَأْ، قَالَ: «مَا أَنَا بِقَارِئٍ»، قَالَ: ” فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي حَتَّى بَلَغَ مِنِّي الجَهْدَ ثُمَّ أَرْسَلَنِي، فَقَالَ: اقْرَأْ، قُلْتُ: مَا أَنَا بِقَارِئٍ، فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي الثَّانِيَةَ حَتَّى بَلَغَ مِنِّي الجَهْدَ ثُمَّ أَرْسَلَنِي، فَقَالَ: اقْرَأْ، فَقُلْتُ: مَا أَنَا بِقَارِئٍ، فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي الثَّالِثَةَ ثُمَّ أَرْسَلَنِي، فَقَالَ: {اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ. خَلَقَ الإِنْسَانَ مِنْ عَلَقٍ. اقْرَأْ وَرَبُّكَ الأَكْرَمُ} [العلق: 2] ” فَرَجَعَ بِهَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَرْجُفُ فُؤَادُهُ، فَدَخَلَ عَلَى خَدِيجَةَ بِنْتِ خُوَيْلِدٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا، فَقَالَ: «زَمِّلُونِي زَمِّلُونِي» فَزَمَّلُوهُ حَتَّى ذَهَبَ عَنْهُ الرَّوْعُ، فَقَالَ لِخَدِيجَةَ وَأَخْبَرَهَا الخَبَرَ: «لَقَدْ خَشِيتُ عَلَى نَفْسِي» فَقَالَتْ خَدِيجَةُ: كَلَّا وَاللَّهِ مَا يُخْزِيكَ اللَّهُ أَبَدًا، إِنَّكَ لَتَصِلُ الرَّحِمَ، وَتَحْمِلُ الكَلَّ، وَتَكْسِبُ المَعْدُومَ، وَتَقْرِي الضَّيْفَ، وَتُعِينُ عَلَى نَوَائِبِ الحَقِّ، فَانْطَلَقَتْ بِهِ خَدِيجَةُ حَتَّى أَتَتْ بِهِ وَرَقَةَ بْنَ نَوْفَلِ بْنِ أَسَدِ بْنِ عَبْدِ العُزَّى ابْنَ عَمِّ خَدِيجَةَ وَكَانَ امْرَأً تَنَصَّرَ فِي الجَاهِلِيَّةِ، وَكَانَ يَكْتُبُ الكِتَابَ العِبْرَانِيَّ، فَيَكْتُبُ مِنَ الإِنْجِيلِ بِالعِبْرَانِيَّةِ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَكْتُبَ، وَكَانَ شَيْخًا كَبِيرًا قَدْ عَمِيَ، فَقَالَتْ لَهُ خَدِيجَةُ: يَا ابْنَ عَمِّ، اسْمَعْ مِنَ ابْنِ أَخِيكَ، فَقَالَ لَهُ وَرَقَةُ: يَا ابْنَ أَخِي مَاذَا تَرَى؟ فَأَخْبَرَهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ خَبَرَ مَا رَأَى، فَقَالَ لَهُ وَرَقَةُ: هَذَا النَّامُوسُ الَّذِي نَزَّلَ اللَّهُ عَلَى مُوسَى، يَا لَيْتَنِي فِيهَا جَذَعًا، لَيْتَنِي أَكُونُ حَيًّا إِذْ يُخْرِجُكَ قَوْمُكَ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَوَ مُخْرِجِيَّ هُمْ»، قَالَ: نَعَمْ، لَمْ يَأْتِ رَجُلٌ قَطُّ بِمِثْلِ مَا جِئْتَ بِهِ إِلَّا عُودِيَ، وَإِنْ يُدْرِكْنِي يَوْمُكَ أَنْصُرْكَ نَصْرًا مُؤَزَّرًا. ثُمَّ لَمْ يَنْشَبْ وَرَقَةُ أَنْ تُوُفِّيَ، وَفَتَرَ الوَحْ


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ مُحَمّد بن صَالِح العُثَيْمِين رحمه الله تعالى



Sahih Al-Bukhari


Mlango wa Mwanzo wa Ufunuo (Wahyi)


Imepokewa kutoka kwa ‘Âisha Radhi za Allah ziwe juu yake Ummul-Mu’minîn (Mama wa Waumini) amehadithia: “Jambo la kwanza aliloanziwa kwalo Mtume katika Wahyi ni ndoto nzuri usingizini. Akawa haoni ndoto ispokuwa huja mfano wa mwangaza wa asubuhi (jinsi ilivyo wazi). Kisha akapendekezewa kukaa pweke. Akawa akiketi katika pango la Hiraa akifanya ibada masiku kadhaa kabla ya kurejea kwa mkewe. Alikuwa akichukua akiba (ya chakula) kwa jambo hilo, halafu akirejea tena kwa (Bibi) Khadija na akichukua akiba kama hiyo. Mpaka akajiwa na Haki (Wahyi) naye yumo katika pango la Hiraa. Akajiliwa na Malaika, akamwambia: Soma. Akasema: Sijui kusoma. (Mtume aeleza): Akanishika na akaniminya mpaka akanifikisha mwisho (wa uchungu). Halafu akaniacha. Akaniambia: Soma. Nikasema: Sijui kusoma. Akanishika na akaniminya mara ya pili mpaka akanifikisha mwisho (wa uchungu). Halafu akaniacha. Akasema: Soma. Nikasema: Sijui kusoma. Akanishika na akaniminya mara ya tatu, kisha akaniacha, akasema: Soma kwa Jina la Mola wako Aliyeumba. Amemuumba Mwanaadamu kwa pande la damu. Soma Mola wako ni Mkarimu sana. [96: 1-3]. Mtume akarejea na Aya hizo huku moyo wake ukitweta. Akaingia kwa Khadija binti Khuwailid Radhi za Allah ziwe juu yake akasema: “Nifinikeni nifinikeni.” Wakamfinika mpaka fazaiko ilipomwondokea. Akamwelezea Khadija kisa kilichompata, akamwambia: “Hakika nilijihofia nafsi yangu. Bibi Khadija akamwambia: Haiwezekani Wallâhi! Allâh Hatokukhizi abadan; kwani wewe unaunga kizazi, unabeba mazito, unawasaidia mafukara, wakirimu wageni na wasaidia katika majanga yanayostahili kusaidiwa. Bibi Khadija akaenda naye hadi kwa Waraqa bin Naufal bin Asad bin Abdil-uzza ambaye ni binamu ya Bibi Khadija. (Waraqa) alikuwa ametanasari zama za ujahiliya, na alikuwa akiandika maandiko kwa Kiibraniya; akiandika Injili kiasi anachojaaliwa na Allâh kuandika. Alikuwa ni mzee mwenye umri mkubwa aliyepofuka. Bibi Khadija akamwambia: “Ewe binamu yangu! Msikilize mpwa wako.” Waraqa akamwuliza: “Ewe mpwa wangu! Waona nini?” Mtume akamhadithia habari aliyoiona. Waraqa akamwambia: “Huyu ndiye Mtunzasiri (Jibril) Aliyeteremshwa na Allâh kwa Mûsâ. Natamani wakati huo (wa kudhihiri Utume) ningalikuwa barobaro. Natamani kama ningalikuwa hai wakati jamaa zako watakapokutoa.” Mtume akauliza: “Wao watanitoa?” Akamjibu: “Ndio. Hakuna mtu yeyote katu aliyekuja na mfano wa uliyokuja nayo ispokuwa hufanyiwa uadui. Iwapo siku hiyo itanifikia, basi nitakunusuru nusra ya nguvu.” Halafu hazikupita siku nyingi, Waraqa akafariki na Wahyi ukasimama.


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.