0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

015. Riyadhu Swalihina Mlango wa Tawba Hadithi ya 03


BUSTANI YA WATU WEMA


وعنْ أبي حَمْزَةَ أَنَس بن مَالِكٍ الأَنْصَارِيِّ خَادِمِ رسول الله صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، رضي الله عنه قال : قال رسول الله صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم

للَّهُ أَفْرحُ بتْوبةِ عَبْدِهِ مِنْ أَحَدِكُمْ سقطَ عَلَى بعِيرِهِ وقد أَضلَّهُ في أَرضٍ فَلاةٍ     متفقٌ عليه

وفي رواية لمُسْلمٍ : « للَّهُ أَشدُّ فرحاً بِتَوْبةِ عَبْدِهِ حِين يتُوبُ إِلْيهِ مِنْ أَحَدِكُمْ كان عَلَى راحِلَتِهِ بِأَرْضٍ فلاةٍ ، فانْفلتتْ مِنْهُ وعلَيْها طعامُهُ وشرَابُهُ فأَيِسَ مِنْهَا ، فأَتَى شَجَرةً فاضْطَجَعَ في ظِلِّهَا ، وقد أَيِسَ مِنْ رَاحِلتِهِ ، فَبَيْنما هوَ كَذَلِكَ إِذْ هُوَ بِها قَائِمة عِنْدَهُ ، فَأَخذ بِخطامِهَا ثُمَّ قَالَ مِنْ شِدَّةِ الفَرحِ : اللَّهُمَّ أَنت عبْدِي وأَنا ربُّكَ، أَخْطَأَ مِنْ شِدَّةِ الفرح


Kutoka kwa Abuu Hamzah, Anas bin Maalik Al-Answaariyy Radhi za Allah ziwe juu yake Mtumishi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema kwamba: Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: [Mwenyezi Mungu Huifurahia mno kwa Tawba ya mja wake kuliko mmoja wenu aliyempata kwa ghafla ngamia wake baada ya kwisha kumpoteza katika ardhi ya jangwa.]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Na katika Riwaya nyingine ya Muslim inasema: [Mwenyezi Mungu Ana furaha mno kwa mja wake wakati anapomuomba Tawba kuliko mmoja wenu aliyekuwa juu ya ngamia wake katika ardhi ya jangwa, akimkimbia naye amebeba chakula chake na maji yake, akakata tamaa kuwa atampata; akauendea mti na akalala kivulini mwake naye ameshakata tamaa ya kumpata ngamia wake. Alipokuwa yuko katika hali hiyo, ghafla akamuona amemsimamia mbele yake, akamshika hatamu yake, halafu akasema kutokana na furaha kubwa: Ewe Mwenyezi Mungu! Wewe ni mja wangu nami ni Mola wako! Amekosea kutokana na furaha kubwa (aliyonayo).]


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله




Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.