0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

012. Riyadhu Swalihina Mlango wa Ikhlas Hadithi ya 12


BUSTANI YA WATU WEMA


عن أبي عَبْد الرَّحْمَن عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ بْنِ الْخطَّابِ، رضي الله عنهما قال: سَمِعْتُ رسول الله صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يَقُولُ: «انْطَلَقَ ثَلاَثَةُ نفر مِمَّنْ كَانَ قَبْلَكُمْ حَتَّى آوَاهُمُ الْمبِيتُ إِلَى غَارٍ فَدَخَلُوهُ، فانْحَدَرَتْ صَخْرةٌ مِنَ الْجبلِ فَسَدَّتْ عَلَيْهِمْ الْغَارَ، فَقَالُوا : إِنَّهُ لا يُنْجِيكُمْ مِنْ الصَّخْرَةِ إِلاَّ أَنْ تَدْعُوا الله تعالى بصالح أَعْمَالكُمْ
قال رجلٌ مِنهُمْ : اللَّهُمَّ كَانَ لِي أَبَوانِ شَيْخَانِ كَبِيرانِ ، وكُنْتُ لاَ أَغبِقُ قبْلهَما أَهْلاً وَلا مالاً فنأَى بي طَلَبُ الشَّجرِ يَوْماً فَلمْ أُرِحْ عَلَيْهمَا حَتَّى نَامَا فَحَلبْت لَهُمَا غبُوقَهمَا فَوَجَدْتُهُمَا نَائِميْنِ ، فَكَرِهْت أَنْ أُوقظَهمَا وَأَنْ أَغْبِقَ قَبْلَهُمَا أَهْلاً أَوْ مَالاً، فَلَبِثْتُ وَالْقَدَحُ عَلَى يَدِى أَنْتَظِرُ اسْتِيقَاظَهُما حَتَّى بَرَقَ الْفَجْرُ وَالصِّبْيَةُ يَتَضاغَوْنَ عِنْدَ قَدَمى فَاسْتَيْقظَا فَشَربَا غَبُوقَهُمَا . اللَّهُمَّ إِنْ كُنْتُ فَعَلْتُ ذَلِكَ ابْتِغَاءَ وَجْهِكَ فَفَرِّجْ عَنَّا مَا نَحْنُ فِيهِ مِنْ هَذِهِ الصَّخْرَة ، فانْفَرَجَتْ شَيْئاً لا يَسْتَطيعُونَ الْخُرُوجَ مِنْهُ
قال الآخر : اللَّهُمَّ إِنَّهُ كَانتْ لِيَ ابْنَةُ عمٍّ كانتْ أَحَبَّ النَّاسِ إِلَيَّ » وفي رواية : « كُنْتُ أُحِبُّهَا كَأَشد مَا يُحبُّ الرِّجَالُ النِّسَاءِ ، فَأَرَدْتُهَا عَلَى نَفْسهَا فَامْتَنَعَتْ مِنِّى حَتَّى أَلَمَّتْ بِهَا سَنَةٌ مِنَ السِّنِينَ فَجَاءَتْنِى فَأَعْطَيْتُهِا عِشْرينَ وَمِائَةَ دِينَارٍ عَلَى أَنْ تُخَلِّىَ بَيْنِى وَبَيْنَ نَفْسِهَا ففَعَلَت ، حَتَّى إِذَا قَدَرْتُ عَلَيْهَا » وفي رواية : « فَلَمَّا قَعَدْتُ بَيْنَ رِجْليْهَا ، قَالتْ : اتَّقِ الله ولا تَفُضَّ الْخاتَمَ إِلاَّ بِحَقِّهِ ، فانْصَرَفْتُ عَنْهَا وَهِىَ أَحَبُّ النَّاسِ إِليَّ وَتركْتُ الذَّهَبَ الَّذي أَعْطَيتُهَا ، اللَّهُمَّ إِنْ كُنْتُ فَعْلتُ ذَلِكَ ابْتِغَاءَ وَجْهِكَ فافْرُجْ عَنَّا مَا نَحْنُ فِيهِ ، فانفَرَجَتِ الصَّخْرَةُ غَيْرَ أَنَّهُمْ لا يَسْتَطِيعُونَ الْخُرُوجَ مِنْهَا
وقَالَ الثَّالِثُ : اللَّهُمَّ إِنِّي اسْتَأْجَرْتُ أُجرَاءَ وَأَعْطَيْتُهمْ أَجْرَهُمْ غَيْرَ رَجُلٍ وَاحِدٍ تَرَكَ الَّذي لَّه وذهب فثمَّرت أجره حتى كثرت منه الأموال فجائنى بعد حين فقال يا عبد الله أَدِّ إِلَيَّ أَجْرِي ، فَقُلْتُ : كُلُّ مَا تَرَى منْ أَجْرِكَ : مِنَ الإِبِلِ وَالْبَقَرِ وَالْغَنَم وَالرَّقِيق فقال: يا عَبْدَ اللَّهِ لا تَسْتهْزيْ بي ، فَقُلْتُ : لاَ أَسْتَهْزيُ بك، فَأَخَذَهُ كُلَّهُ فاسْتاقَهُ فَلَمْ يَتْرُكْ مِنْه شَيْئاً ، اللَّهُمَّ إِنْ كُنْتُ فَعَلْتُ ذَلِكَ ابْتغَاءَ وَجْهِكَ فافْرُجْ عَنَّا مَا نَحْنُ فِيهِ ، فَانْفَرَجَتِ الصَّخْرَةُ فخرَجُوا يَمْشُونَ »       متفقٌ عليه


Kutoka kwa Abu Abdir-Rahmaan, Abdillaah bin ‘Umar bin Al-Khattwaab Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume  akisema: [Waliondoka watu watatu, miongoni mwa watu waliokuwa kabla yenu waliosafiri hadi wakaingia pangoni ili walale. Likaviringika jiwe kutoka juu ya jabali likawafungia pango. Wakasemezana: Hakuna kitakachowaokoa kutokana na jiwe hili isipokuwa mumuombe Allaah kwa ‘amali zenu njema. Mmoja miongoni mwao akaanza kuomba: Ewe Mola, nilikuwa nina wazazi wawili wazee wakongwe, nilikuwa sitangulizi (kabla yao kunywa maziwa) familia wala watumwa. Siku moja haja ya kutafuta kuni ikanipeleka mbali, sikuweza kuwarudia (mapema) mpaka wakalala. Nikawakamulia maziwa yao, nikawakuta wameshalala. Nikachukia kuwaamsha na (nikachukia pia) kuwapa maziwa familia na watumwa kabla yao. Nikawa na (bilauri) imo mikononi mwangu mpaka waamke, hadi alfajiri ikatokeza huku watoto wakipiga kelele kwa njaa miguuni mwangu; wakaamka na wakanywa maziwa yao. Ewe Mola, ikiwa nilifanya hivyo kwa kutaka radhi Zako, basi tufariji katika dhiki tuliyonayo ya jiwe hili. Kukafunguka kidogo kwa namna ambayo hawawezi kutoka.

Mwengine akasema: Ewe Mola, nilikuwa nina bint wa ammi yangu, nilikuwa nikimpenda mno, (Riwaaya nyingine imesema): Nilikuwa nikimpenda kama vile wanaume wanavyopenda mno wanawake. Nikamtaka (kuzini nae), akanikatalia. Mpaka alipokuja mwaka wa ukame, akanijia nikampa dinaar 120 ili niwe nae faragha. Akakubali. Nilipokuwa nimeshamuweza, (Riwaaya nyingine inasema): Nilipoketi baina ya miguu yake akanambia: Muogope Mwenyezi Mungu, na wala usiivunje pete ila kwa haki yake. Nikamuondokea nikiwa nampenda mno (wala sikumfanya chochote), na nikamuachia dhahabu niliyompa. Ewe Mola, ikiwa nilifanya hivyo kwa ajili ya kupata radhi Zako, basi tufariji katika dhiki tuliyonayo. Jiwe likafunguka, lakini walikuwa hawawezi kutoka.

Mtu wa tatu akasema: Ewe Mola, mimi niliwaajiri wafanyakazi, nikawapa ujira wao isipokuwa mtu mmoja, aliuacha ujira wake na akaenda. Nikauzalisha ujira wake mpaka ukawa ni mali nyingi. Baada ya muda akanijia na kuniambia: Ee mja wa Allaah, nipe ujira wangu! Nikamwambia: Kila unachokiona katika ngamia, ng’ombe, mbuzi na watumwa ni ujira wako! Akaniambia: Ee mja wa Allaah, usinifanyie istihzai (shere)!  Nikamwambia: Sikufanyii istihzai. Akachukua mali yote na akayachunga na wala hakubakisha mali yoyote. Ewe Mola, ikiwa nilifanya hivyo kwa kutaka radhi Zako, basi tufariji katika dhiki tuliyonayo. Jiwe likafunguka na huku wakitembea.]    [Imepokelewa na Bukhaariy na Muslim]


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.