0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

006. Riyadhu Swalihina Mlango wa Ikhlas Hadithi ya 06


– وَعَنْ أبي إِسْحَاقَ سعْدِ بْنِ أبي وَقَّاصٍ مَالك بن أُهَيْبِ بْنِ عَبْدِ مَنَافِ بْنِ زُهرةَ بْنِ كِلابِ بْنِ مُرَّةَ بْنِ كعْبِ بنِ لُؤىٍّ الْقُرشِيِّ الزُّهَرِيِّ رضِي اللَّهُ عَنْهُ، أَحدِ الْعَشرة الْمَشْهودِ لَهمْ بِالْجَنَّة ، رضِي اللَّهُ عَنْهُم قال: « جَاءَنِي رسولُ الله صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يَعُودُنِي عَامَ حَجَّة الْوَداعِ مِنْ وَجعٍ اشْتدَّ بِي فَقُلْتُ : يا رسُول اللَّهِ إِنِّي قَدْ بلغَ بِي مِن الْوجعِ مَا تَرى ، وَأَنَا ذُو مَالٍ وَلاَ يَرثُنِي إِلاَّ ابْنةٌ لِي ، أَفأَتصَدَّق بثُلُثَىْ مالِي؟ قَالَ: لا ، قُلْتُ : فالشَّطُر يَارسوُلَ الله ؟ فقالَ : لا، قُلْتُ فالثُّلُثُ يا رسول اللَّه؟ قال: الثُّلثُ والثُّلُثُ كثِيرٌ  أَوْ كَبِيرٌ إِنَّكَ إِنْ تَذرَ وَرثتك أغنِياءَ خَيْرٌ مِن أَنْ تذرهُمْ عالَةً يَتكفَّفُونَ النَّاس ، وَإِنَّكَ لَنْ تُنفِق نَفَقةً تبْتغِي بِهَا وجْهَ الله إِلاَّ أُجرْتَ عَلَيْهَا حَتَّى ما تَجْعلُ في امْرَأَتكَ قَال: فَقلْت: يَا رَسُولَ الله أُخَلَّفَ بَعْدَ أَصْحَابِي؟ قَال: إِنَّك لن تُخَلَّفَ فتعْمَل عَمَلاً تَبْتغِي بِهِ وَجْهَ الله إلاَّ ازْددْتَ بِهِ دَرجةً ورِفعةً ولعَلَّك أَنْ تُخلَّف حَتَى ينْتفعَ بكَ أَقَوامٌ وَيُضَرَّ بك آخرُونَ. اللَّهُمَّ أَمْضِ لأِصْحابي هجْرتَهُم، وَلاَ ترُدَّهُمْ عَلَى أَعْقَابِهم، لَكن الْبائسُ سعْدُ بْنُ خـوْلَةَ « يرْثى لَهُ رسولُ الله صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم» أَن مَاتَ بمكَّةَ »     متفقٌ عليه 


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى





Kutoka kwa Abi Is’haq Sa’ad bin Abi Waqqas radhi za Allah ziwe juu yake mmoja miongini mwa watu kumi waliobashiriwa pepo radhi za ALLAH ziwe juu yao,Anasema “ alinjia Mtume kunitizama mwaka wa hijja ya kuaga kutokana na maradhi yaliyonizidia,nikamwambia: Ewe Mtume wa Mweyezi Mungu hakika yamenifika maumivu haya unayo yaona,na mimi ni mwenye mali mengi na sina wakunirithi isipokuwa binti yangu, je nitoe sadaka thuluthi mbili ya mali yangu? (Mtume ﷺ) akasema la, (usitoe) nikasema je Nusu ewe Mtume wa Mungu? Akasema la.nikasema waonaje Thuluthi ewe Mtume wa Mungu? Akasema (ﷺ) [Thuluthi na hiyo Thuluthi ni nyingi au ni kubwa (kisha akamwambia) hakika wewe kuwaacha warithi wako wenye kujitosheleza ni bora kuliko kuwaacha masikini wanawaomba watu,na Hakika hutatoa nafaka kwa ajili ya kutaka radhi za Mungu ila utalipwa kwa hilo,hata utakacho kiweka katika kinywa cha mke wako.] Akasema: nikasema “Ewe Mtume wa Mungu nitabakia (Makka bada ya kurudi) Wenzangu (Mudina) akasema :[Hutabaki na utakuwa ni mwenye kufanya matendo utakayo taka kwayo radhi za Mwenyzi Mungu ila yatakuzidishia daraja na kukunyanyuwa,na huenda ukabakia mpaka watu wakanufaika na wewe,na wengine wakadhurika kwa ajili yako,(kisha Mtume akaomba) “Ewe Mwenyezi Mungu watimizia Maswahaba wangu hijra yao,wala usiwarudisha nyuma ya visiginyo vyao,Lakini huzuni ni Sa’ad bin Khawalah] anamuombolezea Mtume wa Mwenyezi Mungu” kwa kuwa alifia Makkah.   [Imepokelewa na Bukhari na Muslim.]


SIKILIZA SHEREHE YA HADITHI HII NA DR.ISLAM



SEHEMU YA PILI YA HADITHI HII NA DR.ISLAM



Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.