0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

ZAKA ZA NAFAKA NA MATUNDA

SOMO LA FIQHI

Suali: Ni nini Maana ya Vinavyotoka kwenye Ardhi
Jawabu: Ni Kila kinachotoka ndani ya ardhi, na kinawezekana kunufaika nacho.

Na kinachotoka ndani Ardhini ni Sampuli mbili:

1. Ni Nafaka na Matunda na

2. Madini, na Hazina iliyozikwa Ardhini

Suala: Ni nini Maana ya Nafaka na Matunda
Jawabu: Nafaka ni Kila tembe (mbegu) inayohifadhiwa katika mtama, ngano na mfano wa hii.

Na Maana ya Matunda ni Kila tunda linalohifadhiwa kama tende, na zabibu, na lozi.

Suali: Ni ipi hukmu ya zaka ya Nafaka na Matunda?

Jawabu: Hukumu ya kutoa Zaka ya nafaka na matunda ni wajibu, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَآتُوا حَقَّهُ يَوْمَ حَصَادِهِ}   الأنعام:141

[Na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake]   [Al-An-am: 141]

Na kwa kauli ya Mtume ﷺ:

[فِيمَا سَقَتْ السَّمَاءُ وَالْعُيُونُ أَوْ كَانَ عَثَرِيًّا الْعُشْرُ ، وَمَا سُقِيَ بِالنَّضْحِ نِصْفُ الْعُشْرِ]    رواه البخاري 

[Kwa yaliyo nyunyiziwa (maji) ya mbinguni (yaani mvua) au mito au kama yamemea yenyewe (kama vile hali ya umande) (inafaa mtu atoe) ushuri moja (yaani atoe sehemu moja kwa kumi ya mavuno atakayopata (1/10), Na yaliyonyunyiziwa kwa kumwagiwa maji (na mtu mwenyewe) atatoa nusu ya Ushuri] (yaani atoe sehemu moja kwa tano yamavuno atakayopata (1/20) ]      [Imepokewa na Bukhari]

MAELEZO YA HADITHI

ikiwa mtu ameashughulikia mazao yake kwa kutumia nguvu zake katika kunyunyizia Maji,sawa awe ametumia wanyama au vifaa vya kisasa basi mtu huyo atalazimika atoe nusu ya fungu la kumi,ama ikiwa hakunyunyiza Maji bali ni alitegemea Mvua au umande na kadhalika basi mtu huyo atalazimika atoe fungu la kumu.

Suali: Ni yapi Masharti ya kuwajibika kwa Zaka ya nafaka na matunda?

Jawabu: Masharti ya kuwajibika kwa zaka ya Nafaka na Matunda ni kama ifuatavyo:

1.  Iwe ni katika (mavuno) yanayohifadhika.

Ikiwa si mavuno ya kuhifadhika, na ni mavuno ya chakula chake cha siku basi hakuna Zaka ya kutolewa hapo, kwasababu sio ya kuhifadhiwa hayakuzidi mahitaji yake ya kula kwake kwa kila siku, hivyo basi hayamtoshelezi mahitaji yake; kwa kukosekana utulivu wa kunufaika (na yale mavuno).

2. Iwe ni (mavuno) yanayopimwa.

Na hii iwe ni katika (mavuno) yanayopimwa kwa mizani ili kulinganishwa na saaq, nayo ni kipimo (fulani), hii inaashiria kutambulika kwa mavuno hayo; kwa kauli ya Mtume ﷺ:

[لَيْسَ فِي حَبٍّ وَلا تَمْرٍ صَدَقَةٌ حَتَّى يَبْلُغَ خَمْسَةَ أَوْسُقٍ]     رواه مسلم

[Hakuna katika nafaka, wala tende Zaka yoyote mpaka ifike saaq tano]    [Imepokewa na Muslim.]

[Al – Wasaq: Ni Sawa na Pishi 60.]

Basi ikiwa sio mavuno yanayopimwa kama vile mboga, na mabogaboga, hakuna Zaka kwa vitu hivi.

3. Iwe imemea kwa kupandwa na mtu katika Ardhi yake.

Ama yaliyomea peke yake bila kupandwa na mtu Mavuno hayo hayana Zaka.

4. Mavuno yafikie Nisabu.

Nayo ni Makapu matano, kwa kauli ya Mtume ﷺ:

[لَيْسَ فِيمَا دُونَ خَمْسَةِ أَوْسُقٍ صَدَقَةٌ]    رواه مسلم

[Hakuna katika nafaka wala tende Zaka yoyote mpaka ifike saaq tano]    [Imepokewa na Muslim.]

Na hii itakuwa ni sawa na (Pishi) mia tatu, nayo ni sawa na (612kg) katika ngano nzuri, na yanachanganywa matunda ya aina moja pamoja ya mwaka mzima ili kukamilisha nisabu, kama sampuli tofautitofauti za tende, kwa mfano tende za sukkari zinachanganywa na tende za barhy, kwasababu ni sampuli za mavuno aina moja, wala haifai kuchanganya aina tofauti ya mavuno kwa nyengine, hivyo basi haifai kuchanganya ngano kwa shayir, wala ngano kwa tende.

Sauli: Ni wakati gani wa kuwajibika kutoa Zaka ya Nafaka na Matunda.
Jawabu: Inawajibika utoaji wa Zaka katika nafaka pindi pale zitakapokomaa kuwa tayari, na katika matunda pale yatakapoanza kuonesha uzuri wake, kwa hali ya kwamba yamefikia kuwa mazuri kulika, na atakayeuza matunda au nafaka baada ya wakati wake wa kuwajibika kutolewa Zaka basi Zaka itakuwa ni kwa aliyeuza, kwasababu alikuwa akimiliki mavuno hayo wakati ule wa kuwajibika kutolewa Zaka.

Suali: Nikiwango gani kinachowajibika kwa Zaka ya nafaka na matunda?

Jawabu: Kiwango kinacho wajibika katika Zaka na Nafaka na Matunda na kama ifuatavyo:
1. Yalazimu kutoa ushuri (10%) Kwa (mavuno) ambayo kwamba hayakunyunyiziwa maji Kwa kuenezewa (na mtu) au kwa kugharamika (kwa mtu), kama vile yaliyonyunyiziwa kwa maji ya mvua au mito.

2. Yalazimu kutoa nusu ushuri (5%) kwa yaliyo nyunyiziwa kwa kuenezwa (na mtu) na kugharamika, kama yale yanayo nyunyiziwa kwa maji ya visima.

3. Yalazimu kutoa rubui tatu ya ushuri (7.5%) kwa yaliyo nyunyiziwa kutumia njia zote mbili, kama vile yanayo nyunyiziwa mara nyengine kwa maji ya mvua na mara nyengine kwa maji ya visima.

Na dalili ni kauli ya Mtume ﷺ:

[فِيمَا سَقَتْ السَّمَاءُ وَالْعُيُونُ أَوْ كَانَ عَثَرِيًّا الْعُشْرُ ، وَمَا سُقِيَ بِالنَّضْحِ نِصْفُ الْعُشْرِ]   رواه مسلم

[Kwa yaliyo nyunyiziwa kwa maji ya mbinguni na mito, na maziwa (yatolewe Zaka) ushuri, na kwa yaliyo nyunyiziwa kwa kutumia saania [ Saania: Ni mnyama anayetumika kunyweshea] (yatolewe Zaka) nusu ushuri)]    [Imepokewa na Muslim.]

Suali: Je? kuna Hukmu gani kwa kuharibika kwa Nafaka na Matunda?
Jawabu: Nafaka zikiharibika au matunda bila ya kuharibiwa na mtu au kushindwa kuzichunga vizuri, basi hakuna Zaka kwa mavuno hayo, ikiwa kuharibika kwake baada ya kupita mda wa kuwajibika kwake kwa kushindwa kuzichunga vizuri, au kuyaharibu mavuno kwa kusudi jambo hili halimuondoshei mtu jukumu la kutoa Zaka, atalazimika atekeleze jukumu hili hivyo hivyo.

Suali: Asali inafaa kutolewa Zaka?
Jawabu:  Ameeleze Ibnu Abdulbar (Mungu amrahamu) kwamba Jumuhuri ya wanavyoni kwamba asali haitolewi zaka nahilo ndilo lililo wazi, kwa sababu hakuna dalili katika Qur’ani wala katika Hadithi ya kuwajibisha kuitolewa zaka, na asili nikutowajibika lolote mpaka ipatikane dalili ya kuwajibisha.


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.