0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

YUSUF ESTES

YUSUF ESTES

Skip Estes alizaliwa Ohio mwaka 1944 na kuhamia Texas mwaka 1949. Alikulia katika familia ya Kiprotestant; kama mmoja wa ‘Wanafunzi wa Kristo’ (Disciples of Christ). Skip Estes alikuwa amejizama katika masuala ya kimuziki, burudani, masoko, na aliweza kumiliki makampuni ya muziki ikiwemo The Estes Piano and Organ Company.

Mwaka 1991, Estes alikuwa muislam wakati alipotaka kumbadili Muislamu wa Misri kutoka katika Uislamu kuwa mkristo. Mkewe, baba yake, watoto na mama mkwe nao wakabadili dini kuwa Waislamu. Maelfu ya watu kusilimu yamesababishwa naye kwa nguvu za Mungu na ilishatokea aliweza kusilimisha watu wapatao 135 kwa mkupuo mmoja.

Skip Estes alibatizwa akiwa na umri wa miaka 12 huko Pasadena, Texas. Baba yake, ambaye alikuja kuwa mchungaji wa kuheshimika kanisani miaka ya 1970 alikuwa msaada mkubwa katika kazi za kanisa hasahasa program za shule ya kanisa.

Wazazi wake walikuwa wanafahamiana na wahubiri wengi wa televisheni na hata walidiriki kutembelea Oral Roberts na kusaidia ujenzi wa jengo la ibada “Prayer Tower” huko Tulsa, Oklahoma. Walikuwa wasaidizi wakubwa wa Jimmy Swaggart, Jim na Tammy Fae Baker, Jerry Fallwell, John Haggi na Pat Robertson. Akiwa kijana wa miaka kumi na, Skip alifanya utafiti mkubwa katika dini mbalimbali, kama Ukristo wenyewe, Uhindu, Uyahudi, Metafizikia, Ubudha, Imani ya wale wa asili ya Marekani pasipo kufatilia kuhusu uislam. Alikuja kusema haya yafuatayo bila kutegemewa:

“Cha kushangaza zaidi, neno ‘Utatu’ halipo katika Biblia…niliuliza wachungaji na wahubiri inakuwaje moja ijumuishwe na tatu? Na iweje Mungu mwenyewe ashindwe kusamehe watu mpaka ajifanye binaadamu ashuke duniani watu wake wamtese na ndio hapo awasamehe! Tena ukifikiria kuwa ni Mungu na ndio mwenye uweza wote ulimwenguni kote. Kwa kweli hawakuweza kuja na chochote isipokuwa hoja zisizo za msing na mawazo yao tu.”

Mwanzoni mwa 1991, baba yake Skip alianza biashara na jamaa fulani wa kimisri. Baba yake alimuamuru kuonana nae lakini alisita kwanza kuonana na hao “watekaji, walipuaji, magaidi”. Skip hakuwa na fikra hizo hata siku moja ya kukutana na muislam. “Hatuwezi kumbadilisha huyu mtu kuwa Mkristo, baba” hii ndio sentensi iliyokuwa ikizunguuka kichwani na kinywani mwa Skip. Hivyo akafikiria kutumia njia za panya ili kumbadili huyu mwenza wa baba yake katika biashara kuingia katika Ukristo. Siku waliyopanga kukutana, Skip alibeba silaha zake kama Biblia, msalaba mkubwa unaong’aa na kapelo iliyoandikwa “Yesu ni Mungu”. Baadae Skip alikubali kufanya biashara na Muhammad; hatimaye wakawa muda mwingi pamoja katika safari zao za kibiashara kaskazini mwa Texas. Na ilikuwa katika kipindi hiki ambapo Skip na Muhammad walikuwa wakipenda kujadili mambo yahusuyo imani zao. Skip alikuja kuelewa kumbe Waislamu wanamwamini Yesu kuwa ni Mtume wa Mungu; aliyezaliwa kimaajabu, bila uingiliano na mwanaume, Yesu alikuwa Masihi,; alipaa kuelekea mbinguni, na atarejea tena duniani kabla ya mwisho wa dunia.

Baada ya muda, Skip alimwalika Muhammad kwenda kukaa katika nyumba yao kubwa.

Na mwengine ambae alialikwa nyumbani hapo ni mchungaji wa Kikatoliki ambae amekuwa mmeshenari kwa miaka zaidi ya 12 kasakazini na kusini mwa Amerika, Mexico na mji uitwao Hell’s Kitchen uliopo huko New York.

Nyumbani, walikuwa wanakuwa pamoja katika meza ya chakula baada ya chakula cha jioni kujadili masuala ya kiimani.

Skip analeta toleo lake la Biblia (Revised Standard Version of the Bible) baba analeta King James Version of the Bible, mke wa Skip naye anakuja na toleo tofauti la Biblia bila kumsahau mchungaji akiwa na Biblia ya Kikatoliki ambayo ilikuwa na vitabu 7 zaidi ya Biblia ya Kiprotestanti.

Na tatizo la Biblia ipi ndio sahihi na bora likazuka hapo kila mtu akitoa hoja na mawazo yake.

Wakati walipomuuliza Muhammad kuna aina ngapi za Qur’an, Skip hakuamini masikio yake kusikia kuna Qur’an aina moja tu tena ambayo haijawahi kubadilika tangu alipokuwa mwenyewe Mtume Muhammad.

Akatatizika na kuchanganyikiwa zaidi alipoambiwa tena imehifadhiwa na watu wengi duniani kuanzia ganda la kulia mpaka kushoto.

Siku moja yule mchungaji wa Kikatoliki alimuuliza Muhammad kama ataweza kumpeleka msikitini akajionee ulivyo na akakubaliwa ombi lake.

Siku nyengine Muhammad na yule mchungaji walikwenda tena msikitini lakini sasa walitumia muda mrefu kule. Wakati walipowasili katika nyumba ya Skip, Skip aliweza kumgundua mtu mmoja tu ambae ni Muhammad, hakuweza kumgundua yule wa pembeni ambae alikuwa kavalia kanzu na kofia nyeupe. Na baada ya kumuangalia vizuri akashangaa kuona kumbe ni yule mchungaji. “Peter?” Skip aliita.

“Umekuwa Muislamu?!” Mchungaji alikuwa kashauingia uislam.

Skip akaenda kuongea na mkewe kumuelezea mkasa ule lakini mkewe wake akamchanganya zaidi kwa kumueleza hata yeye anaenda kusilimu kwani aligundua ndio ukweli. Huku akiwa amechanganyikiwa, akashuka chini kwenda kwa Muhammad na kumuomba watoke nje kujadili jambo.

Waliongea usiku kucha na ilipofika asubuhi Skip alikiri uislam ni ukweli.

Haikuishia hapo. Skip aliomba Mungu kutoka moyoni kabisa “Ewe Mungu, niongoze, niongoze”.

Na ilopukuwa takribani mida ya saa 5 asubuhi, Skip alisimama mbele ya mashahidi wawili, Father Peter Jacob, aliyekuwa mchungaji na Muhammad Abdul-Rahman kutamka shahada ya kuingia katika Uislamu. Dakika chache baadae, mkewe akamfata katika Uislamu. Miezi kadhaa iliyofata baba yake naye akaingia katika Uislamu.

Watoto wake wakatolewa katika shule ya Kikristo na kuwekwa shule ya Kiislamu. Nyumba nzima ikabadilika kuwa ya Kiislam. Skip alisema, “Ni kwa Rehma za Mungu tu, wote tuliongozwa kuufata ukweli, tuliondolewa vizibo vilivyo masikioni na upofu uliokuwa umefunika macho yetu na kufuli zilizofunga nyoyo zetu, tunashkuru alituongoza”.

Mwaka 1999, Yusuf Estes alikuwa mjumbe katika Taasisi ya kidini (National Muslim) huko Washington, DC.

Tangia mwaka 2005, Yusuf Estes amekuwa akitokea katika vituo mbalimbali vya televisheni kama IslamChannel, Peace TV,na  Huda TV ambavo ni vituo virushavyo matangazo yake masaa 24 nchi nyingi duniani, kupitia satelaiti na tivuti zake. Pia, amejitolea kuwa imam katika makazi ya jeshi Texas; mwakilishi mteule katika kongamano kwa ajili ya viongozi wa dini la Umoja wa Mataifa lihisulo amani mwaka 2000; amekuwa akiombwa kutoa hotuba mbalimbali katika vyuo vikuu; mwongozaji wa vipindi katika televisheni, mhubiri, ameanzisha tovuti nyingi zenye teknolojia ya hali ya juu zinazohusu uislam, kwa mfano sehemu za watu kuongea katika intanet (chatrooms), kuonana na kuwasiliana (video conferencing), na sehemu za burudani za kiislamu kwa ajili ya vijana (entertainment sites for youth).

Yusuf Estes kashahutubia sehemu zaidi ya mara elfu duniani kote. Baadhi ya hotuba zake na ambazo zinaweza kupatikana katika intaneti bure (mf. http://www.aswatalislam.net au nadeem.lightuponislam.com) ni hizi zifuatazo:

►My Journey to Islam – Before &after Islam (Safari Yangu Kuuelekea Uislam – Kabla na baada ya kusilimu)

►Why Priests and Preachers are Coming to Islam (Kwanini Wachungaji, Makasisi na Mapadri Wanakuja Katika Uislam)

►Purpose of Life (Dhumuni la Kuishi)

►The Beauty of Islam – Understanding why bad things happen to good people (Uzuri wa Uislam – Kwanini vitu vibaya vinawatokea watu wazuri) (*)

** Hii ilikuwa ni Dondoo (excerpt) ya kitabu cha Salim Boss kiitwacho“Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno” chenye kurasa 672 zote zimechapishwa kwa rangi (full colour). Ni tarjama ya kitabu kilichouzika sana kiitwacho “They are Either Extremely Smart or Extremely Ignorant”  Kwa usomaji wa ziada tembelea www.extremelysmart.org au www.facebook.com/muerevumno “**


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.