0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

VITA VYA AL FIJAR

VITA VYA AL-FIJAR 


Wakati Mtume alipofikisha umri wa miaka kumi na mitano vilitokea vita vya Al-Fijar kati ya Makuraishi na wale waliokuwa pamoja nao miongoni mwa Kinana, na Qais ‘Ailan. Kiongozi wa Makuraishi na Kinana alikuwa ni Harb Bin Umayya, kwa sababu ya cheo chake kwao, kwa umri na utukufu. Ushindi ulikuwa ni wa Qais dhidi ya Kinana, mpaka ilipofika katikati ya mchana ushindi ulikuwa ni wa Kinana dhidi ya Qais. Vita hivi viliitwa kwa jina la Al-Fijar, kwa sababu ya kuvunjwa kwa mambo matukufu ya Al-Haram na miezi mitukufu. Vita hivi vilihudhuriwa na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na alikuwa akikusanya mikuki na mishale ya maadui na kuwapa ammi zake waitumie.” 1*


1) Arraheeq Al Makhtum 89

* Mukhmear Siratu Rrasul, Uk. 16. Ibn Hisham, Juzuu 1, Uk. 180-183.

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.