VIGAWANYO VYA MAJI
SWALI: Maji yanagwanyika sehemu ngapi kama walivyo elezea wanachuoni wa fiqhih?
JAWABU: Maji yanagawanyika Viganyo vitatu kwa ujumla kama walivyo elezea wanachuoni wa fiqih kwa itifaki ya madhehebu manne.
Kigawanyo cha kwanza: Ni maji ya kawaida,nao ni maji yaliobaki katika umbile lake,bila ya kubadilika rangi yake, au harufu yake, au tamu yake,kwa kitu ambacho ni vigumu kuepUkana nacho.
Dalili kutoa kwenye Qur’ani:
{وَأَنزَلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً طَهُورًا} الفرقان:48
Mwenyezi Mungu asema:
“Na tumeteremsha kutoka Mbinguni maji Twahara” [Alfuqaan: 48]
Na amesema tena :
{وَيُنَزِّلُ عَلَيْكُم مِّنَ السَّمَاءِ مَاءً لِّيُطَهِّرَكُم بِهِ وَيُذْهِبَ عَنكُمْ رِجْزَ الشَّيْطَانِ} الأنفال:11
[Na akakuteremshieni maji kutoka mbinguni ili kukusafisheni kwayo na kukuondoleeni uchafu wa Shet’ani,” [Al-Anfaal:11]
Na katika hadithi
عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه , عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه قال: [ إن الماء طهور لا ينجسه شيئ] رواه أبوداود والترمذي والنسائي وأحمد
Amepokea Abuu said Al’khudriy Radhi za mwenyezi mungu ziwe juu yake,kutoka kwa Mtume Rehema na amani zimfikie yeye amesema [hakika maji ni twahara na hayanajisiki kwa kitu chochote] [Imepokewa na Abuu Daud na Attirmidhiy,na Annasai,na Ahmad ]
Na hukumu ya maji haya ni twahara yenyewe na waweza kutwahirishia vitu vingine, nao ni kama maji ya mvua, maji ya kisima, maji ya bahari, maji ya barafu, maji chemchem ya ardhi, maji ya zam zam, na maji yalio badilika kwa kitu kilicho zalikana nao.
Kigawanyo cha pili: Ni maji yalio badilika kwa kuingia kitu twahara na kubadilisha rangi yake, au harufu yake, au tamu yake kama vile maji ya waridi,juice, chai, na kadhalika.
Na hukmu ya maji haya huwa ni twahara yenyewe waweza kutumia katika kunywa na kupikia lakini huwezi kutumia katika kujitwahirisha kama vile kutawadha au kuogea.
Kigawanyo cha tatu: Ni maji yalio najisika ,nao ni maji yalio ingia najisi na kubadilisha moja katika sifa zake kama vile tamu yake au rangi yake au harufu yake.
Na hukumu ya maji haya ni haramu kuyatumia kama kunywa, au kupikia na vile vile ni haramu katumia katika mambo ya ibada kama vile kutawadhia, kuogea na kuoshea.
Na baadhi ya wanachuoni wamegawanya maji Vigawanyo viwili tu.
A) Maji twahara: nao ni maji ya kwaida yalio baki katika umbile lake,
B) Maji ya najisi: Nao ni maji yalio ingia najisi na kubadilisha moja katika sifa zake, kama tamu yake, rangi yake, na harufu yake.
Na Allah ndie Mjuzi zaidi