0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

UMOJA KATIKA UISILAMU SEHEMU YA PILI- Hussein ali Omar swidiq

UMOJA KATIKA UISILAMU SEHEMU YA PILI

Tukiendelea na mfululizo wa mazungumzo yetu tulikomea kwenye maneno haya (Kwa hio waislamu ni umma mmoja kwa kuafikiana kwao katika misingi ya itikadi na ya kisheria japo wakitafautiana katika juziiyati (mambo yasio kuwa misingi )….inaendelea

swala litakalo jitokeza, jee ni yapi mambo ambao Waislimu wakiyafanya watautilia nguvu uislmau wao na itakuwa ni sababu ya kupatikana kwa umoja?
Miongoni mwa mambo hayo ni kama yafuatavyo :
1) Kuwa na Itikadi moja .
Itikadi za waisilamu kwa upande wa kumuamini kwao mwenyezi Mungu ni moja kama ilivyo katika misingi ya imaani (nguzo za imani) hakuna tofauti kati yao katika misingi hii ,wote wana amini upweke wa mwenyezimgu (الله وحدانية) uwepo wa Malaaika ,wanaamini Vitabu walivyo teremshiwa manabii walio tangulia,wana amini mitume na manabii walio tangulia,wana amini uwepo wa siku ya mwisho ( siku ya malipo ) na vile vile wanaamini kadar kuwa kheir na shari zinatoka kwa mwenyezimgu. kama mwenyezimgu alivyo lizungumzia hilo katika Qur’ani kwenye sura ya pili aya 285.

Na kama vile ilivyo kuja katika mapokezi mengi sahihi kutoka kwa bwana Mtume ﷺ akilithibisha hilo.
Na hii ndio itikadi ya waislamu wote katika zama zote na yeyote atakae pinga moja katika misingi hio atakuwa ametoka katika mila ya Mislamu ,Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’ani:

{ومن يَكْفُرْ بِالإِيمَانِ فَقَدْ حَبِط عَمَلُهُ وَهُوَ فِي الآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ}     سورة المائدة: 5

[Na yeyote atakae kataa kuamini bila shaka amali yake imepotea naye katika akhera atakuwa mioangoni mwa wenye khasara]    [Al Maida:5]

Ibnu abasi anasema katika kutafsiri maneno haya

Yaani kukataa kuamini ni kule kutoamini aliyo teremshiwa Mtume ﷺ.

Kwa maana hiyo yoyote katika Waislamu akawa na imani tofauti na misingi hii ima akazindisha lolote katika haya au akapunguza chochote hazingatiwi kuwa ni katika Waislamu hata akawa na muonekano wa uislamu .
Kama mfano kwa wale wanao amini kwenye nguzo hii ya kwanza ya imani ambao ni kuamini upweke wa Allah katika kumfanyia yeye ibada,wao wakaigeuza imani hii kuwa msingi wa kukubaliwa matendo ya mwanadamu ni kuamini uwepo wa Maimamu kumi na mbili …wakawafanya maimam hawa ni wasila baina ya mja na mola wake na kwamba Maimamu wana uwezo wa kuweka sheria ya kuhalalisha au kuharamisha.
Kwenye imani ya kuwepo kwa malaika sisi tunaamini kuwa malaika ni viumbe wa Allah wameumbwa kwa Nuru hawamuasi mola kwa lolote na wana fanya walio amrishwa..lakini wao wana amini kuwa malaika wameumbwa kutokana na nuru ya maimamu kumi na mbili na wao (malaika ni watumishi wa maimamu) “Mwenyezi Mungu aliumba kutoka kwenye Nuru ya uso wa Ali Bin Abii Twalib Radhi za Allah Malaika elfu sabiini wakimtakia yeye msamaha na kuwatakia vipenzi vyake .” Biharul anwar 23/320.
Na mengine mengi ambao yapo kinyuma na misingi ya imani.

Kwa hio ili kuupata umoja wa kiislamu kwanza tushikamane kwenye msingi huu wa imani…itaendela…
imeandikwa na

Hussein Ali Omar Swidiq +255717755358.

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.