0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

UJENZI WA MATUMAINI KATIKA JAMII


AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


Mtume () alifanikiwa kusimamisha nguzo za jamii mpya kwa busara na hekima zake.

Bila shaka hali hii iliacha athari kwa Waislamu. Alikuwa akiwaleta katika nuru ya elimu, alizitakasa nafsi zao na akawahimiza kufuata mambo mema na kuwa na mwenendo mzuri. Aidha alikuwa makini kuwafundisha maadili mema na ibada. Muhimu kuliko yote ni Utii kwa Allah () na Mtume (). Ipo siku mtu mmoja
alimwuliza Mtume (), “Matendo yapi bora katika Uislamu?.” Mtume (ﷺ) akajibu; ”Wape watu chakula na toa salamu kwa unayemjua na kwa usiyemjua (1)

Abdullah bin Salam alisema; wakati Mtume () alipofika Madina nilikwenda kumwona, nilipohakikisha kuwa ndiye mwenyewe, nilijua kuwa si mrongo. Maneno ya mwanzo aliyoyasema ni ile ha_dithi yake: “Enyi watu toleaneni salamu, lisheni chakula, ungeni udugu, Salini usiku na hali ya kuwa watu wamelala mtaingia peponi kwa salama. “ (2)

Katika hadithi yake nyingine, amesema; ”Hataingia peponi yule ambaye jirani yake hajasalimika na shari zake” (3)

Akasema; “Mullslamu ni yule ambaye wamesalimika Waislamu wenzake na ulimi wake na mikono yake ” Akasema; ”Hawi Muumini kamili mmaja wenu mpaka ampendelee ndugu yake lile umbalo linaipenda nafsi yake”  (4) Akasema ”Waumini wote ni kama mtu mmoja, likiumwa jicho lake huumwa mwili mzima, na kikiumwa kichwa chake huumwa mwili mzima.”  (5) Akasema; ”Muumini kwa Muumini ni kama jengo moja, kila tofali hutia nguvu tofali jngine”  (6) Akasema; “Msibughudhiane, msihusudiane na msipeane migongo, Enyi waja wa Mwenyezi Mungu kuweni ndugu, si halali kwa Muislamu kumhama ndugu yake zaidi ya masiku matatu” (7)

Akasema;_ ”Muislamu ni ndugu ya Muislamu mwenzake hamdhulumu na hamsalimishi kwa adui; atakayemkidhia haja ndugu yake Muislamu, Mwenyezi Mungu Atamkidhia haja yake, na mwenye kumuondolea Muislamu mwenzake mateso na dhiki Mwenyezi Mungu Atamuondolea matesa ya siku ya Qiyama; na mwenye kumsitiri Muislamu, Mwenyezi Mungu Atamsitiri siku ya Qiyama.” (8) Akasema; ”Wahurumieni walio katika ardhi watawahurumia nyinyi walio mbinguni” (9) Akasema; Si Muumini yule anaeshiba na hali ya kuwa jirani yake ni mwenye njaa ubavuni mwake” (10)  Akasema; ”Kumtukana Muislamu ni kutoka katika utii wa Mwenyezi Mungu na kugombana naye ni ukafiri” (11)
Alifudisha kwa vitendo kuwa, “jumbo la kuondosha uchafu njiani ni Sadaka na jambo hilo huhesabiwa kuwa ni tawi miongoni mwa matawi ya Imani” (12)

Alikuwa akiwahimiza Waislamu kutoa katika mali zao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu () na alikuwa akiwatajia fadhila za kutoa na faida za kiroho zinazopatikana kwa kufanya hivyo. Alikuwa akisema;

”Sadaka huzima makosa na madhambi kama maji yanavyozima moto” (13)
Akasema; ”Muislamu yeyote atakayemvisha nguo Muislamu mwenzake, Mwenyezi Mungu Atamvisha nguo za kijani zilizo peponi. Muislamu yeyote atakayemlisha Muislamu mwenzake aliye na njaa Mwenyezi Mungu (ﷻ) Atamlisha kutoka katika matunda ya peponi; na Muislamu yeyote atakayemnywesha Muislnmu mwenzake aliye na kiu, Mwenyezi Mungu Atamnywesha kutoka
katika mvinyo uliochundiwa” (14) Na akasema; ”Ogopeni moto ijapokuwu kwa kutoa kipande cha tende, na kama hukukipata basi angalau kwa maneno mazuri.” (15)
Pamoja na, yote hayo Mtume () alikuwa akihimiza watu kujizuia na kujichunga na tabia ya kuomba, na akawa anataja fadhila za kusubiri na kutosheka. Alifundisha kuwa kuomba ni dosari kwa mwenye kuoma isipokuwa kama mtu atakuwa hana budi amezidiwa sana.

Kama alivyokuwa akiwazungumzia mambo ya ibada, fadhila na malipo yake kwa Mwenyezi Mungu, alikuwa akiwaletea ushahidi ili kuunganisha mambo ya kiroho na kimwili, kwa mujibu wa wahyi uliokuwa ukishuka kwake kutoka mbinguni.

Alikuwa anawasomea Qur’an ili kuwashajiisha kutekeleza majukumu na wajibu wao na wakati huhuo kutilia mkazo ufahamu na kuzingatia.
Hivyo ndivyo alivyoinyanyua ari yao, matumaini yao, vipaji vyao na akawafunza maadili ya juu na mambo yaliyo bora mpaka wakawa ni sura ya kilele cha juu cha ukamilifu ulioeleweka katika historia ya watu baada ya Mitume.
Abdullah bin Masoud (r.a) amesema;

مَن كانَ مُسْتَنًّا ، فَلْيَسْتَنَّ بمن قد ماتَ ، فإنَّ الحيَّ لا تُؤمَنُ عليه الفِتْنَةُ ، أولئك أصحابُ محمد – صلى الله عليه وسلم –  كانوا أفضلَ هذه الأمة : أبرَّها قلوبًا ، وأعمقَها علمًا ، وأقلَّها تكلُّفًا ، اختارهم الله لصحبة نبيِّه ، ولإقامة دِينه ، فاعرِفوا لهم فضلَهم ، واتبعُوهم على أثرهم ، وتمسَّكوا بما استَطَعْتُم من أخلاقِهم وسيَرِهم ، فإنهم كانوا على الهُدَى المستقيم

“Mwenye kutaka kufuata basi na awafuate Wale walio kufa kwani ni vigumu kwa aliye hai kusalimika na fitna, hao ni Masahaba wa Muhammad (s.a.w) walikuwa ni wabora wa umma huu, wema zadi kwa nyoyo na wajuzi zaidi kwa elimu zao. Mwenyezi Mungu (s.w.t) Aliwachagua wao ili wawe masahaba wa Mtume Wake na wasimamishaji wa Dini Yake, kwa hivyo jueni ubora wao na fuateni nyayo zao, na shikamaneni na zile ambazo mnaziweza katika tabia zao, na mwenendo wao, kwani wao walikuwa kwenye uongofu
ulionyoka.” (16)
Mtume () alikuwa ni mwenye kusifika kwa sifa za kitabia zilizo wazi na anasifika kwa ukamilifu wa vipaji na matendo mazuri, mambo yaliyofanya watu wampende na wawe tayari kumpigania na kujitolea uhai wao kwa ajili yake. Kila alipotamka Masahaba wake walifanya haraka kutekeleza aliloagiza, ilikuwa hatoi maelekezo yoyote au uongozi wowote isipokuwa walishindana katika kujipamba na mambo
hayo. »
Kwa msingi huu Mtume () aliweza kujenga katika mji wa Madina jamii mpya iliyo bora na iliyotukuka na ambayo imefahamika katika historia. Aliweza kuyapatia ufumbuzi matatizo yote ya kijamii. Kuwafanya watu wafaidike na wastawi kutokana na ufumbuzi huo kwa kuhisi raha baada ya kuwa wametaabika kwa muda mrefu kwa sababu ya giza totoro lililokuwa limewafunika.
Kwa mfano wa mambo kama haya ya kiimani na yaliyo makubwa ilikamilika misingi ya kuijenga jamii mpya ambayo ilipambana na kila mawimbi na matatizo kwa kipindi kirefu mpaka mwisho wa uelekeo wake, na ikaugeuza mapito ya masiku na historia.


1) Sahihil Bukhari, Iuzuu 1,Uk. 6, 9.
2) Ttirmidhi, Ilm Majah na Darimy. Mishkatu Masabiih, Juzuu 1, Uk. 168.
3) Muslim, Mishkatu Masabiih, Juzuu 2, Uk. 422
4) Sahihul Bukhari, Iuzuu 1, Uk. 6.
5) Muslim, Mishkatu Masabih, juzuu 2, Uk. 422
6) Bukhari na Muslim, Mishkatu Masabih, Juzuu 2, Uk.422
7) Sahihul Bukhari, Iuzuu 1, Uk. 6.
8) Sahihul Bukhari, Muslim Miskaul masabihh Juzuu 2, Uk. 422
9) Sunan Abu Daud, Juzuu 2, Uk. 235. Iami’u Ttirmidhy, Juzuu 2, Uk. 14.
10) Bayhaqi, Mishkatul Masabih, Juzuu 2, Uk. 424.
11) Sahihil Bukhari, Iuzuu 2, Uk. 893.
12) Bukhari na Muslim, Mishkatul Masabih, Iuzuu 1, Uk. 12, 167.
13) Ahmad, Ttirmidhy, Ibn Majah, Mishkatul Masabih, Juzuu 1, Uk. 14.
14) Sunan Abu Daud, ]ami’u Ttirmidhy, Mishkatul Masabih, Juzuu 1, Uk. 169.
15) Sahihil BukI1ari,]uzuu 1, Uk. 190, Iuzuu 2, Uk. 890.
16) Amepokea Razin, Mishkatul Masabih, Juzuu 1, Uk. 32.

Begin typing your search above and press return to search.