AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Tumetangulia kueleza kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) alifika Madina, kwa Banu Najjari, siku yaIjumaa tarehe kumi na mbili, Rabiul Awwal, mwaka wa 1 A. H, sawa na tarehe na saba, Mwezi wa Tisa, 622 C.E., na kuwa yeye nyumba ya Abu Ayyub na akasema, ”Hupa ndio mashukio ambayo Amependa Mwenyezi Mungu (ﷻ)”, kisha akahamia kwenye nyumba ya Abu Ayyub.
Ujenzi wa Msikiti wa Mtume
Hatua ya kwanza ambayo Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) aliichukua baada ya yote hayo ni kuujenga Msikiti pale mahali‘ Ambapo ngamia wake alipiga magoti. Aliamrisha kujengwa Msikiti baada ya kununua eneo kutoka kwa vijana wawili mayatima, ambao walikuwa wanamiliki. Katika ujenzi wake yeye mwenyewe kwa kubeba matofalj, na mawe huku akisema;
اللَّهُمَّ إنَّه لا خَيْرَ إلَّا خَيْرُ الآخِرَهْ… فَبَارِكْ في الأنْصَارِ وَالمُهَاجِرَهْ
“Ewe Mala Wangu wa Haki hakuna maisha isipokuwa maisha ya akhera, wabarikie Muanswari na Muhujirina.”
Alikuwa akisema:
هذا الحِمالُ لا حِمالَ خَيْبَرْ *** هذا أبَرُّ رَبَّنا وأَطْهَرْ
Hii Indiyo mizigo ya kuchukuliwa, siyo mizigo ya Khaibar,
Hii ndiyo nzuri. Mwema sana _ee Mala wetu na iliyosafi sana
Jambo hili liliongeza sana uchangamfu wa Masahaba katika ujenzi mpaka ikafikia hatua ya mmoja wao kusema;
لئن قعدنا والنبيُّ يعملُ لذاك منَّا العملُ المضلِّلُ
Iwapo tutakaa na hali ya kuwa Mtume (ﷺ) anafanya kazi, hicho kwetu sisi kitakuwa ni kitendo cha upotofu. ”
Kafika ardhi hiyo palikuwepo makaburi ya Mushirikina na yalikuwapo pia magofu, mitende na miti ya Gharqad. Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) aliamrisha makaburi ya Mushirikina kufukuliwa, magofu yakasawazishwa, mitende na miti mingine ikakatwa ikapangwa katika sehemu ya mbele ya Msikiti. Qibla kilielekea upande wa Baitul Muqaddasi. Na zilikuwa mbao zake mbili za pande mbili za mlango ni za
mawe, zilisimamishwa kuta za Msikiti kwa matofali na udongo na uliezekwa kwa mbao na nguzo za magogo. Sakafu yake ilitengenezwa kwa changarawe na mawe madogo madogo. Milango ya Msikiti ilikuwa mitatu na urefu wake ulikuwa, katika ile sehemu ambayo inakiandamia Qibla mpaka mwisho wake, ni yadi mia moja na zile sehemu mbili ni mfano wa hivyo au chini yake, na msingi wake ulikaribia
yadi tatu.
Mtume (ﷺ) alijenga nyumba za mawe na matofali pambezoni mwake na aliziezeka kwa makumbi na magogo, na hivyo vilikuwa ni vyumba vya wake zake Mtume (ﷺ); na baada ya kukamilika vyumba hivyo alihamia hapo kutoka katika nyumba ya Abu Ayyub. (1)
Msikiti haukuwa ni mahali pa Swala tu, bali ulikuwa ni chuo kikuu, Waislamu wakipata mafundisho ya Uislamu na Itikadi. Ndani ya Msikiti walikutana na kuzoeana watu wa makabila mbalimbali, ambayo kwa muda mrefu walikuwa mbalimbali kwa sababu za kijahilia na vita vilivyokuwepo kati yao.
Msikiti ulikuwa ndio kituo cha kuendesha mambo yote ya Waislamu, na pahala pa kufikishiana taarifa mbalimbali na ulikuwa ni bunge la kufanya vikao vya kushauriana na utekelezaji. Pamoja na yote hayo Msikiti wa Mtume (ﷺ) ulikuwa ni nyumba ambayo iliwahifadhi idadi kubwa ya mafakiri.— wengi wao Waislamu ambao walihajir kutoka Makkah – ambao hawakuwa na nyumba za kukaa, mali, wake
wala watoto.
Katika siku za mwanzo za Hijra iliwekwa sheria ya kuadhini, kwa siku mara tano, adhana ambayo hutetemeka kwa sababu yake nyoyo za waumini wa kweli Ulimwenguni kote. Kisa cha ndoto ya Abdillah bin Zaidi bin Abdi Rabb kilichopokelewa na Tirmidhy, Abu Dawud, Ahmad na Ibn Khuzaima kuhusu adhana ni maarufu.(2)