Ulifika wakati Saad bin Muadhi aliondoka Madina kuelekea Makka kwa madhumuni ya kwenda kutekeleza
ibada ya Umrah na alipofika huko alifikia kwa Umayya bin Khalaf, akasema kumwambia Umayya; “Niangalilie muda mzuri usio na ghasia ili nikatufu na nikaizunguuke Al-Ka’aba kwa nafasi.” Akatoka naye wakati wa mchana, huko akakutana na Abu Jahli ambaye alimwuliza; ”Ewe Abu Swafwan ni nani huyu uliye pamoja naye?.’ Akajibiwa; Ni Saad.’ Abu Jahli akasema, ”Ninakuona unatufu Makka na hali ukiwa katika amani na hali huko kwenu mmewahifadhi watu ambao wameacha dini yetu na mmedai kuwa nyinyi
mnawasaidia; Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kuwa kama usingekuwa pamoja na Abu Swafwani, usingerejea kwa watu wako salama.” Saad akamjibu kwa sauti kali bila woga, ”Kwa jina la Mwenyezi Mungu iwapo utamzuia na jambo hili basi na mimi nitakuzuia wewe na jambo ambalo ni kubwa
kwako kuliko hili, nalo ni njia yako ya kuelekea Madina. (1)
Makuraishi Wanawatisha Muhajirina
Makuraishi walipeleka ujumbe kwa Waislamu wakiwaambia: ”Msihadaike kuwa eti mmesalimika kwa
kutoka kwetu kwenda Yathrib. Tutakuja, tutawamaliza na tutayaharibu mafanikio yenu kwenye mji wenu.”(1)
Makamio haya hayakuwa ya maneno matupu, yalithibitika kwa Mtume ((ﷺ) ) kwa vituko vya Makuraishi.
Makuraishi walifanya mambo mengi katika kuikusudia shari. Mambo ambayo yalimlazimisha Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) kutokuupitisha usiku amelala, isipokuwa kukesha akiwa kafika ulinzi pamoja na Masahaba wake.
Katika Sahihi Muslim, amepokea kutoka kwa Aisha (Radhi za Allah ziwe juuu yake.) kuwa
alisema: ”Baada ya kufika kwake Madina usiku mmoja Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) alikesha na akasema; ’Natamani kungekuwa na mtu mwema miongoni mwa Masahaba zangu ili anilinde usiku huu. Aisha (Radhi za Allah ziwe juuu yake) akaendelea kusema: ’Wakati sisi tumo katika hali hiyo ghafla tukasikia mshindo wa silaha.’ Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) akamwuuliza Saad bin Abi Waqass,
Jambo gani limekuleta?.’ Akasema: ’Nilikhofu mtu asije akakudhuru, kwa hiya nimekuja kukulinda. Mtume wa Mwenyezi Mung (ﷺ) akamwombea dua kisha akalala. (3)
Ulinzi huu ulikuwa wa kuendelea. Imepokewa kutoka kwa Aisha (Radhi za Allah ziwe juuu yake),
Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) alikuwa akilindwa usiku mpaka ilipoteremka kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:
“وَاللَّهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ”
”…Na Mwenyezi Mungu Atakulinda na watu…” (5:67) ‘
Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) alichungulia nje akiwa Quba akawaambia, ”Enyi watu nendeni zenu, hakiki Mwenyezi Mungu Ananilinda. ” (4)
Maisha ya Mtume (s.a.w) hayakuwa hatarini tu, bali njama za maadui zilikusudiwa Waislamu wote. Imepokewa na Ubayi bin Kaabi (Radhi za Allah ziwe juuu yake), Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) na
Masahaba wake walipofika Madina walihifadhiwa na Anéwar, na walikuwa na ulinzi wa kutosha.’ Mtume (s.a.w) aliwafanya wakawa wamoja na wakawa wanawapiga maadui zao wakati mmoja na silaha zao zikiwa tayari kwa mapigano wakati wowote ule.