0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

SWALA YA KUOMBA MVUA

SWALA YA KUOMBA MVUA

Kila ugonjwa una tiba yake, ardhi ikiwa kavu na kupatikana ukame. Uislamu umeweka ibaada Maluum nayo ni  (Swalatul IstisQai) ni Swala ya kumuomba Mwenyezi Mungu kuteremsha mvua. Leo Swala hii imesahulika kabisa katika Umma wa kislamu. Waislamu wakipata matatizo ya uhaba wa Mvua, moja kwa moja wanaelekea kuomba majini na mashetani. Mafundisho ya Mtume(Swalla Llahu ‘alayhi wasallam  yako wazi kabisa kuwaelekeza Waislamu katika njia ya Allah Subhaanahu wa Taala)wakati wowote na hali yoyote sawa wakati wa raha au shida. Kumtii Mwenyezi Mungu ndio mambo yote. Amesema Mwenyzi Mungu(Subhaanahu wa Taala:

{وَلَوْ أَنَّهُمْ أَقَامُوا التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْهِم مِّن رَّبِّهِمْ لَأَكَلُوا مِن فَوْقِهِمْ وَمِن تَحْتِ أَرْجُلِهِم ۚ مِّنْهُمْ أُمَّةٌ مُّقْتَصِدَةٌ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ سَاءَ مَا يَعْمَلُونَ}

Na lau kuwa wangeli ishika Taurati na Injili na yote waliyo teremshiwa kutokana na Mola wao Mlezi, basi hapana shaka wangeli kula vya juu yao na vya chini ya miguu yao. Wapo watu miongoni mwao walio sawa, lakini wengi wao wanayo yafanya ni mabaya mno.”     [Al-Maaida:66]

Na Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

{أُحِلَّ لَكُمْ صَيْدُ الْبَحْرِ وَطَعَامُهُ مَتَاعًا لَّكُمْ وَلِلسَّيَّارَةِ ۖ وَحُرِّمَ عَلَيْكُمْ صَيْدُ الْبَرِّ مَا دُمْتُمْ حُرُمًا ۗ وَاتَّقُوا اللَّهَ الَّذِي إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ}     {الأعراف:96}

Na lau kuwa watu wa miji wangeli amini na wakamchamngu, kwa yakini tungeli wafungulia baraka kutoka mbinguni na katika ardhi. Lakini walikanusha basi tukawapatiliza kwa sababu ya yale waliyo kuwa wakiyachuma”      [Al-A’raaf:96]

Kumuasi Mwenyezi Mungu ndio sababu ya kuleta shari na kuondoka kwa baraka.

Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

{ وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَىٰ مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ}    آل عمران:135

Na ambao pindi wafanyapo uchafu au wakajidhulumu nafsi zao humkumbuka Mwenyezi Mungu na wakamwomba msamaha kwa dhambi zao – na nani anaye futa dhambi isipo kuwa Mwenyezi Mungu? na wala hawaendelei na waliyo yafanya na hali wanajua.”     [Al-Imraan:135]

Ametaja Ibn Qayyim (R.A) baadhi ya maafa yanayoletwa na maasi; huleta udhalifu, huharibu akili, huwaondosha haya, hudhoofisha moyo, huondosha neema, hutia maradhi moyo, huleta nuksi, hupotosha ya moyo, hufanya moyo kuwa mdogo, huondosha karama, pia Baraka, na kulaumiwa, kutishika, huondosha hima ya kumcha Mwenyezi Mungu.

Ukame ni alama ya kuwa watu mbali na twaa ya Mwenyezi Mungu, na ishara ya kuzidi maasi. Hali ya anga inabadilika kutokana na maasi.

Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

{ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِي النَّاسِ لِيُذِيقَهُم بَعْضَ الَّذِي عَمِلُوا لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ}  الروم:41

Ufisadi umedhihiri bara na baharini kwa iliyo yafanya mikono ya watu, ili Mwenyezi Mungu awaonyeshe baadhi ya waliyo yatenda. Huenda wakarejea kwa kutubu.       [Al-Ruum:41]

Na anasema Anas bin Malik: (R.A.) Upepo ukiwa mkali hujulikana hilo kwa uso wa Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam.

Amepokea Abu Huraira (R.A) hadithi: kutoka kwa Mtume(Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)akisema: [Hakisimami Qiyama mpaka iondoke ilimu, na kuzidi Zilzaal, na zahama kuwa karibu, na kudhihiri fitna, na kuzidi mauaji, mpaka itakua kwenu mali nyingi]. Ufupisho ni kujirudi nafsi, na kuomba msamaha kwa Allah pamoja na kufuata sheria za Allah(Subhaanahu wa Taala).

Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

 { يُنَبَّأُ الْإِنسَانُ يَوْمَئِذٍ بِمَا قَدَّمَ وَأَخَّرَ  بَلِ الْإِنسَانُ عَلَىٰ نَفْسِهِ بَصِيرَةٌ  وَلَوْ أَلْقَىٰ مَعَاذِيرَهُ}       القيامة:13-15

Siku hiyo ataambiwa aliyo yatanguliza na aliyo yaakhirisha. Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake. Na ingawa atatoa chungu ya udhuru.”   [Al-Qiyama:13-15]

Na neno lake Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam akisema:  [Tunajilinda na Mwenyezi Mungu kutokana na uovu wa nafsi zetu, na uovu wa matendo yetu].

Imepekewa kwa Masahaba wakisema: Alitusalisha Mtume(Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)swala ya usubuhi Hudeibiyah kukiwa na mawingu usiku, baada ya hapo akatukabili na kusema: Je mnajua alivyosema Mwenyezi Mungu? Wakajibu maswahaba: Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanajua. Akasema Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam: [Baadhi ya waja wangu wamekua waumini ni wale waliosema tumeteremshiwa mvua kutokana na fadhila zake Mwenyezi Mungu, na makafiri tumeteremshiwa mvua kutokana na nyota fulani].

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.