SHUBHA YA KURITADI KWA MASWAHABA
Mashia wanadai kuwa Maswahaba waliritadi baada ya kufa Mtume Muhammad na hakuthubutu katika uislamu ila wachache na katika hoja yao hiyo wanaitolea dalili aya ya Mwenyezi Mungu aliyetukuka:
وما محمدٌ إلا رسول قد خلت من قبله الرسل أفئن مات أو قتل انقلبتم على أعقابكم ومن ينقلب على عقبيه فلن يضر الله شيئاً وسيجزي الله الشاكرين. ” آل عمران آية 144
“Na Muhammad hakuwa ila ni Mtume tu. Wamekwisha pita kabla yake Mitume. Je, akifa au akauwawa ndiyo mtageuka mrudi nyuma? Na atakaye geuka akarudi nyuma huyo hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu atawalipa wanao mshukuru” [Al-Imraan:144]
Wanasema kuwa aya hii yaonyesha wazi kuwa Maswahaba wataritadi baada ya kufa Mtume ila wachache wenye kuwa na shukrani ,kama alivyo sema Mwenyezi Mungu:
{وقليل من عبادي الشكور} [سورة سبأ آية 13]
“Ni wachache katika waja wangu wanao shukuru” [Saba’i:13]
Jawabu:
Kwanza kabisa yaonyesha wazi ujinga na kutoelewa kwa wanaosema maneno hayo. Lau angesoma kitabu chochote cha tafsiri na kuangalia sababu ya kuteremka aya hii hawangesema walio yasema.
Aya hii imeteremka siku ya vita vya Uhud wakati walipo pata waislamu waliyo yapata kwa kuuliwa Maswhaba sabiini na kupasuliwa uso Mtume wa Mwenyezi Mungu na kuvunjwa meno yake. Pia watu kueneza uvumi kuwa Mtume ameuliwa,hapo ndipo baadhi ya wanafiki waliposema ikiwa Mtume Muhamad ameuliwa basi regeeni katika dini yenu ya kwanza yaani ushirikina ndio ikateremka aya hii
{وما محمدٌ إلا رسول قد خلت من قبله الرسل أفئن مات أو قتل انقلبتم على أعقابكم ومن ينقلب على عقبيه فلن يضر الله شيئاً وسيجزي الله الشاكرين}[سورة آل عمران آية 144]
“Na Muhammad hakuwa ila ni Mtume tu. Wamekwisha pita kabla yake Mitume. Je, akifa au akauwawa ndiyo mtageuka mrudi nyuma? Na atakaye geuka akarudi nyuma huyo hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu atawalipa wanao mshukuru”
[Al-Imraan:144]
Amepokea imam Al-Twabariy kwa Isnadi yake katika tafsri yake kutoka kwa Al-Dhwahak amesema katika neno lake Mwenyezi Mungu:
{وما محمد إلا رسول قد خلت من قبله الرسل}
“Na Muhammad hakuwa ila ni Mtume tu. Wamekwisha pita kabla yake Mitume.’
Watu walio kuwa na shaka na maradhi na unafiki walisema siku watu walipomkimbia Mtume na kupasuliwa juu ya uso wake na kuvundwa meno yake,Muhamad ameuliwa rudini kwenye dini yenu ya kwanza, hilo ndilo neno lake Mwenyezi Mungu:
{أفئن مات أو قتل انقلبتم على أعقابكم}
Je, akifa au akauwawa ndiyo mtageuka mrudi nyuma? [Tafsiri Al-Twabariy 3/458]
Kwa hivyo aya iliteremka juu ya wanafiki walio eneza uvumi kwa kuuliwa Mtume na kutaka Maswhaba Warudi kwenye ushirikina dini ya mababu zao.
Wala aya haijazungumzia kabisa kuhusu Kuritadi Maswahaba baada ya kufa Mtume kama wanavyo dai Mashia.
Pili: Hata aya kama imeteremka juu ya Maswahaba baada ya kufa Mtume itakuwa ni dalili ya wazi kuwatakasa Maswahaba kwani wao ndio walio anda jeshi lakupigana na Murtadina.
Abubakar Swidiq na Maswahaba ndio walio simama imara kupigana na walio ritadi mpaka akawarudisha kwenye dini na wale walio kataa kurudi aliwapiga,na hili laonyesha wazi ubora wa swahaba wa Mtume (S.W.A).hasa Abubakar na Fadhla yake juu ya kuitetea dini hii.
Ndio imepokewa kwa sayyidnya Ali radhi za allah ziwe juu yake katika neno lake Mwenyezi Mungu:
{وسيجزي الله الشاكرين}
“Na Mwenyezi Mungu atawalipa wanao mshukuru”
[الثابتين على دينهم أبا بكر وأصحابه]
“Wenye na thabati juu ya dini yao, Abubakar na Maswahaba wake” [Tafsiri Al-Twabariy 3/455].
Ndugu Muislamu tazama hawa Mashia namna wanvyogeuza aya za Mwenyzi Mungu bila ya kujali wala kumuogopa Mwenyezi Mungu.
Wamewasingizia maswahaba wa Bwana Mtume Muhamad kuwa waliridadi baada ya kufa kwake ilhali hawa Maswahaba ndio walio simama imara kupigana na walio ritadi mpaka kuwamaliza na Uislamu kuenea ulimwengu Mzima.
Na hawa Maswahaba Allah amewasifu kwenye kitabu chake kitukufu,na wao ndio walio isambaza hii dini mpaka kutufikia sisi, na hili liko wazi kwa kila mwenye akili na fahamu mzuri lakini hawa mashia chuki zao juu ya Maswahaba wamebadilisha mazuri yao kuyafanya mabaya,na kuwabadikia ubaya badala ya uzuri.