Ruhusa ya Kupigana
Mazingira haya ya hatari yalikuwa yanatishia kuwepo kwa Waislamu pale Madina. Makuraishi waliendelea na uovu na uasi wao dhidi ya Waislamu. Mwenyezi Mungu Mtukufu
(s.w.t) Aliwapa Waislamu ruhusa ya kupigana na Makafiri. Mwenyezi Mungu (s.w.t) Amesema:
” أُذِنَ لِلَّذِينَ يُقَاتَلُونَ بِأَنَّهُمْ ظُلِمُوا ۚ وَإِنَّ اللَّهَ عَلَىٰ نَصْرِهِمْ لَقَدِيرٌ”
”Wameruhusiwa (kupigana) wale wanaopigwa, kwa sababu wamedhulumiwa. Na ’yaqini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa Kuwasaidia.” (22:39)
Mwenyezi Mungu (s.w.t) Aliteremsha Aya hii kutoa maelekezo ya kufuata ili kuondosha kila aina ya uovu na upotofu na kusimamisha alama za Dini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t). Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema:
الَّذِينَ إِن مَّكَّنَّاهُمْ فِي الْأَرْضِ أَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ وَأَمَرُوا بِالْمَعْرُوفِ وَنَهَوْا عَنِ الْمُنكَرِ ۗ وَلِلَّهِ عَاقِبَةُ الْأُمُورِ
” Wale ambao tukiwapa madaraka katika nchi husimamisha Swala, na wakatoa Zaka, na wakaamrisha mema, na wakakataza mabaya. Na kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo ya mambo yote.” (22:41)
Bila shaka ruhusa ya kupigana ilishuka Madina na siyo Makka, isipokuwa wakati wenyewe wa kushuka haufahamiki. Idhini ya kupigana ilitolewa na ilikuwa ni hekima katika mazingira kama haya (ambazo chanzo chake ni uasi na ukorofi wa Makureishi). Waislamu kuwa na uwezo wa kudhibiti njia ya biashara ya Makuraishi inayotokea Makka kwenda Sham. Mtumb wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) ilibidi
achague kati ya mawili:-
(1) Mpango wa kwanza: Kufunga mikataba ya kunusuriana na kutofanyiana uadui na makabila ambayo yalikuwa jirani na njia hiyo au yaliyokuwa yanaishi kati ya njia hii na Madina.
Tumekwisha kuutanguliza mkataba wake Mtume (ﷺ) pamoja na Mayahudi. Vile vile alifunga mkataba wa
kunusuriana na kutofanyiana uadui pamoja na kabila la Juhaina kabla ya kuingia katika harakati za kijeshi. Makazi yao yalikuwa yako kafika vituo vitatu, kutoka Madina, na alifunga mkataba wakati wa doria zake za kijeshi na litafafanuliwa zaidi.
(2) Mpango wa Pili: Akaweka utaratibu wa kupeleka kikosi kimoja baada ya kingine kwenye njia hii, kwa ajili” ya doria.