Nguzo za Imani (Arkaan al-Imaan) Nguzo 6 za Imani kwa Mpangilio:
1. Kuamini Mwenyezi Mungu (Allaah)
Ushahidi kutoka katika Qur’an:
” ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡحَيُّ ٱلۡقَيُّومُۚ “
Mwenyezi Mungu! Hapana mungu ila Yeye, Aliye Hai, Msimamizi wa kila kitu…” [Surat Al-Baqarah](w), 2:255)
Ushahidi kutoka katika Hadith: Kutoka kwa ‘Umar Radhi za Mwenyeezi Mungu ziwe juu yake ambaye amesema:
فَأَخْبرني عن الإِيمان. قال: [أَن تُؤمِنَ باللهِ، وملائِكَتِهِ وكُتُبِهِ، ورسُلِهِ، واليَوْمِ الآخِرِ، وتُؤمِنَ بالْقَدَرِ خَيْرِهِ وشَرِّهِ]
Niambie kuhusu Imani. Akasema (Mtume Rehma na amani zimfikie yeye) [Ni kumwamini Mwenyeezi-Mungu, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Yake na siku ya Qiyaama, na kuamini ya kuwa kheri na shari zinatoka Kwake (Allaah alie tukuka ]….” (Hadith ndefu ya Jibril, [Sahih Muslim](w))
2. Kuamini Malaika wa Mwenyezi Mungu
Ushahidi kutoka katika Qur’an:“
بَلۡ عِبَادٞ مُّكۡرَمُونَ لَا يَسۡبِقُونَهُۥ بِٱلۡقَوۡلِ وَهُم بِأَمۡرِهِۦ يَعۡمَلُونَ
… Bali hao (wanao waita wana) ni watumwa walio tukuzwa. Hawamtangulii kwa neno, nao wanafanya amri zake. [ Surat Al-Anbiyaa 21:26-27 ]
Dalili kutoka Hadith: …na uwaamini Malaika wa Mwenyezi Mungu.. (Hadith ya Jibril – Muslim)
3. Kuamini Vitabu vya Mwenyezi Mungu
Ushahidi kutoka katika Qur’an:
{ نَزَّلَ عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ بِٱلۡحَقِّ مُصَدِّقٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَأَنزَلَ ٱلتَّوۡرَىٰةَ وَٱلۡإِنجِيلَ }
Amekuteremshia Kitabu kwa haki, kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake. Na aliteremsha Taurati na Injili .” [Surat Aal Imran, 3:3]
Ushahidi kutoka katika Hadith: “…na vitabu Vyake…” (Hadith ya Jibril – Muslim)
4. Kuamini Mitume wa Mwenyezi Mungu
Ushahidi kutoka katika Qur’an:
{ وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا رُسُلٗا مِّن قَبۡلِكَ }
“Hakika Tumewatuma Mitume kabla yako… [Surat Ghafir 40:78]
Ushahidi kutoka katika Hadith:
…na Mitume Wake…” (Hadith ya Jibril – Muslim)
5. Kuamini Siku ya Mwisho (Qiyama)
Ushahidi kutoka katika Qur’an:
وَٱلَّذِينَ يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ يُؤۡمِنُونَ بِهِۦۖ وَهُمۡ عَلَىٰ صَلَاتِهِمۡ يُحَافِظُونَ
“Na wenye kuamini Akhera wanakiamini hichi, nao wanazihifadhi Sala zao” [Surat Al-An’am 6:92]
Ushahidi kutoka katika Hadith:
“…na kuamini Siku ya Mwisho…” (Hadith ya Jibril – Muslim)
6. Kuamini Qadar (maisha ya kudura) kheri na shari yake
Ushahidi kutoka katika Qur’an:
“Hakika sisi tumemuumba kila kitu kwa Qadar (kudura). ” [Surat Al-Qamar 54:49 ]
Ushahidi kutoka katika Hadith: “…na kuamini Qadar – kheri na shari yake.” (Hadith ya Jibril – Muslim) —
Hitimisho:
Nguzo hizi sita ndizo msingi wa imani ya Muislamu. Mtu hawezi kuwa na imani sahihi mpaka azikubali zote kwa pamoja.