Nguzo Tano za Uislamu (Arkanul-Islaam)
1. Kushuhudia kuwa hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, na kwamba Muhammad ni Mtume Wake. (Shahada: Laa ilaaha illaLlaah, Muhammadun RasuluLlaah)
Dalili ya Qur’ani:
{شَهِدَ ٱللَّهُ أَنَّهُۥ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ وَأُوْلُواْ ٱلۡعِلۡمِ قَآئِمَۢا بِٱلۡقِسۡطِۚ}
“Mwenyezi Mungu, na Malaika, na wenye ilimu, wameshuhudia kuwa hakika hapana mungu ila Yeye, ndiye Mwenye kusimamisha uadilifu; ” [Aali ‘Imran 3:18]
Na Dalili ya Hadithi: Mtume ﷺ alisema:
[ بُنِيَ الإسْلَامُ علَى خَمْسٍ: شَهَادَةِ أنْ لا إلَهَ إلَّا اللَّهُ وأنَّ مُحَمَّدًا رَسولُ اللَّهِ، وإقَامِ الصَّلَاةِ، وإيتَاءِ الزَّكَاةِ، والحَجِّ، وصَوْمِ رَمَضَانَ ]
“[Uislamu umejengwa kwa nguzo tano:Shahada kuwa hakuna Mola apasaye kuabudiwa isipokuwa Allaah na Muhammad ni Mjumbe wake, kuswali, kutoa Zaka, kuhiji (Makka) na kufunga Ramadhan.]” [ Imepokelewa na Bukhari na Muslim]
2. Kusimamisha Swala (Sala) Kuswali swala tano kila siku kwa wakati wake.
Dalili ya Qur’ani:
{ وَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَۖ إِنَّ ٱلصَّلَوٰةَ تَنۡهَىٰ عَنِ ٱلۡفَحۡشَآءِ وَٱلۡمُنكَرِۗ}
“Simamisha Swala, hakika Swala humzuilia (mtu) na mambo machafu na maovu…” [Al-Ankabut 29:45]
Dalili ya Hadithi: Mtume ﷺ alisema:
“Tofauti kati ya mtu na ukafiri ni kuacha swala.” [ Imepokewa na Muslim ]
3. Kutoa Zaka ( Kuwapa mafakiri na wenye haki mali maalum kila mwaka kwa wenye uwezo.
Dalili ya Qur’ani:
{ وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَۚ }
” Na simamisheni Swala na toeni Zaka” [Al-Baqara 2:110]
Dalili ya Hadithi:
” Na kutoa Zaka…” [Bukhari na Muslim] (sehemu ya hadithi ya nguzo tano)
4. Funga Mwezi wa Ramadhani (Saumu) ( Kufunga kuanzia alfajiri hadi machweo kwa mwezi mzima wa Ramadhani.)
Dalili ya Qur’ani:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُتِبَ عَلَيۡكُمُ ٱلصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُمۡ لَعَلَّكُمۡ
“Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu.” [Al-Baqara 2:183]
Dalili ya Hadithi:
…na kufunga Ramadhani… [Bukhari na Muslim]
5. Kuhiji Nyumba Takatifu ya Allah (Hija) Kufanya ibada ya Hija kwa mwenye uwezo angalau mara moja maishani.
Dalili ya Qur’ani:
{ وَلِلَّهِ عَلَى ٱلنَّاسِ حِجُّ ٱلۡبَيۡتِ مَنِ ٱسۡتَطَاعَ إِلَيۡهِ سَبِيلٗاۚ }
“Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea.” [Aali ‘Imran 3:97]
Dalili ya Hadithi:
…na kuhiji Nyumba Takatifu ya Allah kwa mwenye uwezo. [Bukhari na Muslim]
Hitimisho:
Nguzo hizi tano ni msingi wa maisha ya Muislamu. Mtu hawezi kuwa Muislamu wa kweli bila kuzifuata. Zinatuongoza katika imani, ibada, maadili na mafanikio ya duniani na akhera.