0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

NANI ANALAZIMIKA KUMLEA NA KUMPA MATUMIZI MTOTO WA ZINAA ?

NANI ANALAZIMIKA KUMLEA NA KUMPA MATUMIZI MTOTO WA ZINAA ?

Suali :
Jee Mama aliyepata Mimba ya Zina anapata ujira , ama kujitolea kwake kote kwa ajili ya kumzaa mtoto hakuna faida ? Ikiingia katika hayo ni mali ambayo atamuwekea mtoto ? Na jee ujira wa kuzaa kutokana na zinaa ni kama kuzaa kupitia mimba ya halali ? Na matumizi ya mtoto huyo itakuwa juu nan?

Jawabu :
Kwanza
Akitubia binti kutokana na Zinaa basi (Aliyetubia kutokana na dhambi ni kama mtu asiye na dhambi) kama ilivyokuja katika hadithi ya mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake , imepokelewa na Ibnu Maajah (4250) na ameisahihisha Albaany.
Kwa hivyo mwanamke atakae tubia kutokana na zinaa , basi inatarajiwa yanayompata katika mashaka na tabu za mimba na kunyonyesha na kumlea mtoto mpaka mwisho yote hayo ni katika yanayomfutia madhambi , na anapata thawabu ikiwa atasubiri na akatarajia thawabu ya hayo kutoka kwa Menyezi Mungu..
Amesema Shaikhul Islam Ibnu Taymiyyah Allah amrehemu.
“Yanayomfilkia katika misiba , inafuta madhambi” Amesema Mwenyezi Mungu :

مَا أَصَابَ مِنْ مُصِيبَةٍ إلَّا بِإِذْنِ اللَّهِ وَمَنْ يُؤْمِنْ بِاللَّهِ يَهْدِ قَلْبَهُ

(Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu huuongoa moyo wake.).
Pili :
Ni wajibu kwa mama kumshughulikia na kumlisha mtoto wake aliyemzaa kutokana na zinaa ikiwa anaweza .
Amesema Ibnu Qudaamah : “Kukiwa na uzito kwa baba basi ni wajibu kwa mama kutoka nafaqah na matumizi ya mtoto na hatarudi nae kwake akiwa amepata uepesi” imeisha kutoka katika kitabu cha “Al Mughny” (11/373).
Hii ni katika hali mtoto yuko na baba lakini baba ni fakiri , Je ikia Mtoto hana baba : basi bila shaka matumizi ya mtoto yatakuwa juu ya mama.

Na ikiwa Mama hana mali , basi matumizi ya mtoto huyo ni juu ya warithi wake , kama vile ndugu zake upande wa mama , na Bibi yake upande wa mama.

Na kama sio hivyo , basi matumizi ya mtoto ni juu ya Aswaba wa mama , nao ni baba yake , na ndugu zake , na watoto wa ndugu zake , na Ammi zake na watoto wa Ammi zake .


Begin typing your search above and press return to search.